MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka
50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan,
2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa
mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni
Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka,
Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi,
Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa
katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo
litajumuisha filamu za kitanzania peke yake (Bongo movies)
ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema
katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF
litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa
siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea
kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve
Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya,
Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show
kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani
watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete
sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR)
au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa
udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV
kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena
No comments:
Post a Comment