BARUA YA WAZI KWA WAHESHIMIWA MARAIS DAKTA. J .M. KIKWETE NA DAKTA.
A .M.SHEIN
YAH: KUWAOMBA
MLINUSURU BUNGE LA KATIBA MPYA LITIMIZE LENGO KUSUDIWA
Tafadhalini waheshimiwa husikeni na ombi la hapo juu
mkiwa wakuu wa taasisi ya siasa ya umma au umma wa Taifa letu, ninyi si serikali
wala wakuu wa vyama vyenu tu.
Inaonekana Mungu
ameamua kutukomboa dhidi ya adui yetu mkuu ukoloni mamboleo aliyetajwa mwaka
1967, bila ya ufafanuzi wake. Adui huyu yumo ndani yetu na ndani ya mifumo yetu
ya maisha ,uongozi na utawala kwa ngazi ya Taifa na bara letu. Tusipomuondoa
anaweza kuturudisha kwenye ukoloni au utumwa wa awali polepole.
Mungu anajua kuwa chini ya adui huyu hatuwezi
kuyatimiza malengo ya uhuru wetu tuliyoyataja mwaka 1961,1964 na 1967 hata tukiwa chini ya uongozi na
utawala wa chama kingine. Anafahamu kuwa tuliarifiwa juu ya uwepo wa adui huyu
bila ya ufafanuzi, huenda wasemaji hawakumfahamu
vema adui huyu kwa vile nao walikuwa kundi la pili la wafuasi wa waasisi wa
harakati za kuutafuta uhuru wetu waliomjua vema adui huyu.
Kama alivyowafanya waliotangulia, Mungu anawainua
ninyi bila ya kulijua lengo la kuzianzisha harakati za awamu ya tatu ya
ukombozi wetu dhidi ya adui huyu, anawaongoza kuanzisha mchakato wa kulikagua
Taifa letu toka tulikoanzia, tuone tulipopotelea tujikosoe tutunge na kuandika
katiba mpya itakayotuongoza katika harakati za ukombozi wetu bila ya kuijali
baadae yenu, kwa amani na utulivu wenye
mshikamano na umoja. Ndio maana mwaka 2002
tukiwa AMALI NGO tuliishawishi serikali na WHO wakatunga sheria no 23.
ya mwaka 2003 ya tiba asili, tulikuwa tunatengeneza ufunguo wa kuingilia
alikofichwa adui huyu. Tuko tayari kutoa elimu ya kina kwa umma, uongozi na
serikali dhidi ya adui huyu na harakati hizi nzito.
Amewajaza hekima, busara na upendo kwa Taifa
letu, mkautumia ufunguzi wa bunge la katiba mpya kuyavua madaraka na ushawishi
wa uraisi ,serikali ,vyama vya siasa, tume na uandishi wa rasimu za katiba mpya,
mataifa ya nje taasisi za dini, asasi za kiraia na mtu mmoja mmoja mbele ya
bunge la katiba mpya ; sote tuwe watoa maoni yenye mifumo ya hoja zijadilike
kwa maridhiano, hivyo ndivyo waraka wa kisiasa au katiba ya taifa
itakavyopatikana
Hili bunge maalumu tofauti na mabunge ya kawaida,
litakuwa na wajumbe bila ya miswada,waraka wa rasimu ya pili ya katiba mpya
utakuwa waraka wa maoni kiongozi yaliyowekwa kwenye mifumo ya hoja yaongoze
mijadala. Mfumo huu unawataka wajumbe kuwa wamoja waingize mambo
yaliyosahaulika au yasiyoandikwa kwenye rasimu au kuleta maoni mbadala yakiwa
kwenye mifumo ya hoja ili kwa hekima na busara zao waunde katiba bora.
Kwa bahati mbaya harakati za awamu ya tatu ya
ukombozi wa Taifa letu zilizofichwa ndani ya mchakato wa uandishi wa katiba
mpya hazikutangazwa pamoja nao, huenda siri hii ya Mungu haijajulikana. Hivyo
wajumbe wa bunge hili waliuona mchakato huu ni zawadi kwa muungano wetu
kutimiza miaka 50 tunatafuta namna mpya ya ugawanaji mamlaka na madaraka ya
taifa letu au tunatafuta aina mpya ya maisha au ustawishaji taifa. Katika mvutano
huu wa fikra walijenga misimamo iliyowagawa, rasimu waliigeuza kuwa mswada
baada ya maoni kiongozi; ukawa na wenyewe, wapinzani na waliotupwa nje. Kwa
kuwa tendo hili ni nje ya taratibu za bunge hili
wakajikuta kila upande ukitoa matamko yasiyoweza kujadilika badala ya kutoa
hoja za matamko hayo ambazo zingewapeleka hadi kwenye viini vya matakwa yao
kama vile BMZ, SMZ, TAMISEMI na kadhalika; kasoro hii imelifanya kundi moja
liamue kujitoa bungeni.
Kwa kuwaambia siri ya Mungu aliyoificha kwenye
mchakato huu naamini sasa mtakuwa mmeelewa kuwa kinachotarajiwa kufanywa hapa
ni zaidi ya katiba. Tunataka wajumbe wabakie wamoja wajenge nguvu ya utaifa na
rasimu iwe maoni kiongozi ili yaruhusu maoni mapya yatakayojadiliwa sambamba na
maoni kiongozi kwa nyanja husika, ikibidi hekima, busara , sheria na sera
tulizoziacha za waasisi wetu tuziite katika kuifanikisha siri iliyofichwa
kwenye mchakato huu. Hivyo natarajia wajumbe wote bila ya makundi wala misimamo
au masharti nawasihi mrudi bungeni mkalijenge upya taifa letu msahau mliyonayo.
Nimeigundua siri hii katika utafiti nilioufanya toka
mwaka 1987 -2002 nikitafuta kiini cha vikwazo vya taifa letu tajiri kwa utalii,
rasilimali na mali asili, vipaji vya sayansi na ufundi mbali ya vya
ustareheshaji, ardhi bora na kubwa yenye uzalishaji wa kutosha, lakini hatujitoi kwenye umasikini,
tunazidi kuwa tegemezi sasa hatuna siasa / dira, uongozi na serikali ya kitaifa
, nyumba za kulaza watumishi, viwanda na kadhalika, pia kwa kukikana Kiswahili hadi
leo taifa halijarudishwa kwa wananchi waliowengi maarifa tunayoyapata kwenye
mataifa ya nje hatuyafikishi kwa wananchi waliowengi yakatuletea maendeleo,
hatujui aina /mfumo wa elimu bora kwetu yakutukwamua tulipokwama, mbali ya hayo
adui huyu ameharibu dhana yetu ya uwazi uwajibikaji, na ushirikishwaji kwa kupunguza mamlaka ya raia dhidi ya
uongozi wao na uongozi dhidi ya utawala /serikali yao kunakozaa rushwa ,ufisadi,
ulegevu wa ulinzi wa mipaka, kupoteza huduma kwa umma, kujinyima fedha kitaifa
na kadhalika.
Mambo haya niliyawasilisha juu juu kwa taifa kupitia ITV mnamo tarehe 26/04/2012: mada: NINI TANZANIA, ASILI NA HALI YAKE
MIAKA 48. Tarehe 30 /04/2012: mada: TOFAUTI
YA ELIMU YA UZALENDO NA ELIMU YA URAIA na tarehe 27/03/2914: mada: UGUMU WA KUUNGANISHA SERIKALI ZA
TAIFA LETU; naziona serikali za jamuhuri
ya muungano wa Tanzania na TAMISEMI za kiraia lakini BMZ na SMZ za kijeshi, vipi zote zitakuwa za kiraia ziwe na sura
moja ziunganishwe? Adui huyu kwa miaka yote amewazuia viongozi wetu kulirekebisha
hili kiasi inaonesha CCM ina serikali ya
muungano na tamisemi ya Tanganyika /Tanzania bara lakini upande wa Zanzibar /
Tanzania visiwani hupata wawakilishi kutokaBMZ
wenye serikali SMZ na kuwaingiza kwenye
bunge na serikali ya muungano.
Kwa ufafanuzi huu wa kitafiti ni wazi watanzania
wote sasa tutajua tunachotarajiwa kufanya kwa ajili ya salama yetu, kumshukuru Mungu kwa ufunuo huo ni kwa
wajumbe wote kurudi bungeni na tulionje tuwasaidie, maana hii ni vita dhidi ya
adui yetu mkuu ukoloni mamboleo ila tujue adui huyu hakuumbwa ameundwa/kubuniwa
na watu kwa maslahi yao. Wajumbe mkija na msimamo, mkisusa bunge, mkikataa
kujadili yaliyonje ya rasimu, mtakuwa mnamsaidia adui huyu na waliomuunda
kutekeleza malengo yao na kuliangamiza taifa na bara letu
J4mindu@gmail.com , 0753746479, 0787746479
mindujr3@gmail.com , 0719554564,
Wenu mtiifu
J
.A. Mindu`
Mgunduzi,
m/kiti wa AMALI NGO na mhandisi
No comments:
Post a Comment