(
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw.
Yusuph Mwenda(katikati) akisikiliza jambo toka kwa Ofisa Mkuu wa kitengo cha
Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kulia) muda mfupi kabla
ya kuzindua rasmi duka jipya la Vodacom lililopo Shamo Tower Mbezi
beach gorofa ya kwanza jana jijini Dar es
Salaam.

Yusuph Mwenda akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa
duka la Vodacom Tanzania lililopo Shamo Tower Mbezi beach gorofa ya kwanza
jijini Dar es Salaam,wengine kulia ni Meneja wa duka hilo,Bw.Kartic Subramaniam
na kulia ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom
Tanzania,Bw.Hassan Saleh.
Mkuu wa kitengo cha
Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bi.Pendo Richard (kulia) akimuelezea
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda matumizi ya baadhi
ya bidhaa zinazopatikana katika duka jipya la kampuni hiyo,Mara baada ya Meya
huyo kuzindua duka hilo jana Shamo Towers gorofa ya kwanza, Mbezi Beach jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa kampuni
hiyo,Bw. Hassan Saleh.
· Upatikanaji wa huduma za Vodacom wazidi
kurahisishwa
Dar Es Salaam 17
Novemba 2013… Katika kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wateja wake na
kuwaridhisha kwa kile wanachokihitaji, Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza
Tanzania Vodacom imezindua duka jipya ambalo litawawezesha wateja mbalimbali wa
kampuni hiyo wakiwemo wakazi wa Mbezi Beach kunufaika na upatikanaji wa karibu
wa huduma mbalimbali za muhimu za mawasiliano.
Mgeni rasmi katika
ufunguzi huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewaasa
wakazi wote wa Mbezi kutumia ipasavyo duka hilo ili kuweza kutatua matatizo yao
ya huduma za kimawasiliano.
”Najua walio wengi
walikua wakisubiria na kutamani kuona ni muda gani Vodacom itawaletea duka
ambalo litawapa huduma mbali mbali za kimawasiliano, sasa kuanzia leo duka
limefunguliwa rasmi hivyo mnapaswa kulitumia ipasavyo kwani limewekwa hapa
kwaajili yenu wote wateja wa Vodacom”. Alisema
Mwenda aliongeza kuwa “Idadi kubwa ya watanzania ambao ni
watumiaji wa huduma za kimawasiliano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, hivyo
kufuatia uzinduzi huo itakuwa ni suluhu tosha ya kuwawezesha wateja walioko
Mbezi Beach na hata nje kuweza kutatua haja zao pale wanapokuwa wanahitaji
huduma”.
Kwa upande wake Ofisa
mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh
amesema kampuni yake inatambua mchango unaoendelea kutolewa na wateja wake,
hivyo inazidi kuwaunga mkono kwa kuwapa urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa
kuwafungulia duka ambalo litawawezesha wakazi wa Mbezi kutokupoteza muda wao
mkubwa kwenda mbali kwaajili ya huduma mbalimbali za Vodacom, badala yake
kutatua matatizo yao hapo hapo Mbezi Beach katika duka hilo.
“Mahitaji ya huduma
kwa wateja sasa ni makubwa na watanzania wanahitaji kupata kile
watakachokifurahia katika maisha yao ya kila siku. Hivyo Vodacom kupitia duka
hilo itawawezesha wakazi wa Mbezi na maeneo mengine kuwa karibu na upatikanaji
wa huduma na kuacha kwenda mbali kama walivyokuwa wakifanya apo awali” Alisema
Saleh
Akiongezea kuwa “Bado
tutaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu kwa kuzidi kufungua maduka
mengi zaidi sehemu mbalimbali ambazo hazijafikiwa na kuhakikisha wateja wetu
wote wanaendelea kufurahia huduma zetu za Vodacom, hatimaye kuendelea kubaki
kinara kwa kuwapa huduma bora wateja wetu”
Hadi sasa Vodacom
inamiliki maduka 72 yaliyo katika sehemu mbalimbali za nchi ambayo yanaendelea
kutoa huduma bora na zinazostahili kwa wateja wake kitendo ambacho kinawafanya
kuwa ni kampuni inayoongoza hapa nchini.
Upanuzi huu wa wigo wa
huduma za mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji
kwenye mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya
mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania.
Mwisho…

No comments:
Post a Comment