Mshindi wa Pikipiki
katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania
Bi.Hellen Kilawe akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano
wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa
washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha
taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa
promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
Mshindi wa Pikipiki
katika promosheni ya Timka na Boda Boda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania
Bw.Shadrack Moses Pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni
hiyo,Bw.Matina Nkurlu wakihakiki kadi ya pikipiki wakati wa
makabidhiano yaliyofanyika katika Stoo za ofisi hiyo zilizoko Shekilango jijini
Dar es Salaam. Pikipiki 25na fedha taslimu zilikabidhiwa kwa wakazi wa Dar es
Salaam na Pwani. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
Mshindi wa Pikipiki
katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na kampuni ya Mawasiliano
ya Vodacom Bw.Joseph Mambo akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja
Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi
pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na
fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine
wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfungia kamba ya kofia
ngumu”Helmet”Mshindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda Bw.Joseph Mambo, Katika
Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi
hao.anaeshuhudia kushoto ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid
Maggid.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipanda kwenye pikipiki
yake aliyoshinda katika promosheni hiyo huku akisaidiwa na Meneja Uhusiano wa
Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kulia)wakati wa Hafla ya
kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya
pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni
washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipunga mkono wakati
akiondoka na pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kushoto)wakati wa Hafla ya
kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya
pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni
washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda
15544.
·
Washindi 25 wa
Timka na Boda Boda.
·
Washindi 12 walamba
Milion kumi na sita
·
Neema zaidi kuendelea
kumiminika.
Dar es Salaam,
19th Novemba, 2013….Baada ya washindi
zaidi ya 125 kujishindia Boda Boda na wengine kuendelea kujishindia fedha
taslimu kila siku kutoka kampuni ya simu ya Vodacom ambazo ni zaidi ya milioni
430 zilizotengwa ndani ya siku 100. Vodacom Tanzania kwa mara nyingine tena
katika kuhakikisha inabadili maisha ya kila mteja wake imekabidhi Boda Boda kwa
washindi 25 ambao ni wakazi wa mkoa Dar Es Salaam na
Pwani.
Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania, Matina
Nkurlu amewashauri watanzania wote kuzidi kuendelea kushiriki katika promosheni
hiyo inayoendelea kwa kasi zaidi ya miezi mitatu. Aliendelea na kusisitiza kuwa
Kampuni yake imejidhatiti kuhakikisha haipo mbali na wateja wake kwa kuendelea
kuwanufaisha kwa kuwapa Boda Boda ambazo zitakuwa ni si tu kuwasaidia kwa
usafiri bali ni msingi mzuri katika kuendeleza biashara
zao.
”Kampuni yetu ipo kumnufaisha kila mmoja na imepania
vikali kuhakikisha kila mtanzania anapata msingi ambao anaweza kutumia katika
kuendeleza biashara zao, kwani siku hizi biashara ya Boda Boda imekuwa ni
mwokozi kwa walio wengi ambao huongeza kipato chao kupitia biashara hiyo na ndio
maana sisi Vodacom tumetenga piki piki zenye gharama ya kitanzania shilingi
bilioni 1 kwaajili ya wateja wetu wote nchini” alisema
Matina
Akiongezea kuwa “Kila mmoja anatamani kuwa na msingi
ambao utamuwezesha aweze kuwa na biashara yake ambayo itamuingizia kipato
matokeo yake kujikwamua katika hali ya kiuchumi, hivyo basi ni wakati wa kila
mmoja kunufaika na promosheni mbali mbali zinazazotolewa na kampuni yetu, na
ningependa kuendelea kuwashauri wateja wote wanaoshiriki na wanaoanza kushiriki
kuzidi kuendelea kwani ni haki ya kila mtanzania kujishindia boda boda kutoka
Vodacom”
Ili kuweza kuwa mmoja kati ya washindi kutoka
promosheni hiyo ya Timka na Boda Boda ni rahisi sana, wateja wote wa Vodacom
wanatakiwa kushiriki kwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda namba
15544.
No comments:
Post a Comment