image in blog

image in blog
mindu

Saturday, December 28, 2013

Celebrate CHRISTMASS with DIAMOND PLATNUMZ


1513329_663010003721897_726683344_n
Finaly!!!!!!……….I hope We ushacheza na kuimba saaaaana na Diamond… sasa hii ni maalum kwa Mtoto wako, Mdogo, Ucle, Aunty yako inshort Family!…ni this wednesday 25/12/2013 Christmass katika kiwanja cha Leaders Club, itamwagwa Michezo yooooote ya watoto ikiambatana na Burudani Kali toka @Wcb_wasafi ….ZINGATIA! Kuna kitu cha RedCarpert Maalum kabisa kwajili ya Watoto, hivyo hakikisha mwanao UnaMnyukisha vyakutosha!… Mvalishe kama Diamond, Aimbe kama Diamond, Acheze kama Diamond, Ikiwezekana hata nywele Kiduku cha njano kama Diamond…. Kwani nini si nini ama????? Sponsored by @Cocacolatz watoto Dressed by @babyishtz cC @iviewstudios

(Photo’s) Jiachie na camera ya DJCHOKA pande za DAR LIVE katika sikukuu ya Xmas


4d75c10e6d9811e3a70412937c060170_8???REDCARPET3 REDCARPET6 REDCARPET15 REDCARPET19 REDCARPET26

DIAMOND AFURAHI NA WATOTO KATIKA SHOO YAKE ILIYOANDALIWA NA YEYE

IMG_0756 IMG_0819 IMG_0995 IMG_1009 IMG_1039

Sunday, November 24, 2013

Video: Hii ndio reality show ya Wema Sepetu "In My Shoes" episode ya kwanza




Reality show ya Muigizaji Wema Sepetu inayoitwa "In My Shoes" imeshaanza na hivi ndivyo baadhi ya vitu alivyovizungumzia: 

mama yake alipomzaa aligua sana mpaka akalazwa.
ukiacha Mungu mtu anaempenda ni mama yake mzazi.
mtu wake wa karibu katika familia yake ni dada yake wa kwanza.
amegombana na dada yake nampaka sasa hawaongei.
kusemwa vibaya ama kuandikwa vibaya kwake anachukulia kama challenge.
anaamini kuwa uchawi upo ila hapendi kujihusisha nao.
anaamini alishawahi kurogwa.
amewahi kuwa na mahusiano na wanaume wanne mpaka watano au sina inawezekana.
mimi na diamond tuli connect na tulikuwa na crazy chemistry, alinitumia message kwenye facebook kuwa ananipenda.
siku tatu baada ya yeye kutoka jela ilikuwa ni kama nightmare kwake.
Martine Kadinda ni manager wake lakini pia ni rafiki yake.
Peti Man na Tinny Dady ni watu wake wakaribu wanamjua vizuri
 
click here to see:
 

Wafahamu watanzania wanne walioingia kwenye orodha ya matajiri 50 wa Afrika-2013


 Rostam Aziz aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, Said Bakhresa na mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji wameingia kwenye orodha ya Forbes ya watu 50 matajiri zaidi barani Afrika.

Rostam Aziz ndiye aliyeibuka kidedea kwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1 na kukamata nafasi ya 27 kwenye orodha hiyo.

Huku Mwenyekiti na mtendaji wa makampuni IPP,Reginald Mengi ameshika nafasi ya 34 akiwa na utajiri wa dola Milioni 550  kwenye orodha hiyo.......

 Kwenye nafasi ya 38 ya orodha hiyo, imeshangaza kuona Said Salim Bakhresa na Mohamed Dewji wakiwa sawa kwa utajiri wa dola milioni 500 kila mmoja.

Friday, November 22, 2013

MINDU JR..... THE FUTURE: (News) Vodacom yazidi kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma zake

 

(

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw. Yusuph Mwenda(katikati) akisikiliza jambo toka kwa Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kulia) muda mfupi kabla ya kuzindua  rasmi duka jipya la Vodacom lililopo Shamo Tower Mbezi beach  gorofa ya kwanza jana jijini Dar es Salaam.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw. Yusuph Mwenda akikata utepe  ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa duka la Vodacom Tanzania lililopo Shamo Tower Mbezi beach gorofa ya kwanza jijini Dar es Salaam,wengine kulia ni Meneja wa duka hilo,Bw.Kartic Subramaniam na kulia ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh.

Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bi.Pendo Richard (kulia) akimuelezea Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda matumizi ya baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka jipya la kampuni hiyo,Mara baada ya Meya huyo kuzindua duka hilo jana Shamo Towers gorofa ya kwanza, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo,Bw. Hassan Saleh.

·        Upatikanaji wa huduma za Vodacom wazidi kurahisishwa
Dar Es Salaam 17 Novemba 2013… Katika kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wateja wake na kuwaridhisha kwa kile wanachokihitaji, Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza Tanzania Vodacom imezindua duka jipya ambalo litawawezesha wateja mbalimbali wa kampuni hiyo wakiwemo wakazi wa Mbezi Beach kunufaika na upatikanaji wa karibu wa huduma mbalimbali za muhimu za mawasiliano.
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewaasa wakazi wote wa Mbezi kutumia ipasavyo duka hilo ili kuweza kutatua matatizo yao ya huduma za kimawasiliano.
”Najua walio wengi walikua wakisubiria na kutamani kuona ni muda gani Vodacom itawaletea duka ambalo litawapa huduma mbali mbali za kimawasiliano, sasa kuanzia leo duka limefunguliwa rasmi hivyo mnapaswa kulitumia ipasavyo kwani limewekwa hapa kwaajili yenu wote wateja wa Vodacom”. Alisema
Mwenda aliongeza kuwa “Idadi kubwa ya watanzania ambao ni watumiaji wa huduma za kimawasiliano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, hivyo kufuatia uzinduzi huo itakuwa ni suluhu tosha ya kuwawezesha wateja walioko Mbezi Beach na hata nje kuweza kutatua haja zao pale wanapokuwa wanahitaji huduma”.
Kwa upande wake Ofisa mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh amesema kampuni yake inatambua mchango unaoendelea kutolewa na wateja wake, hivyo inazidi kuwaunga mkono kwa kuwapa urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa kuwafungulia duka ambalo litawawezesha wakazi wa Mbezi kutokupoteza muda wao mkubwa kwenda mbali kwaajili ya huduma mbalimbali za Vodacom, badala yake kutatua matatizo yao  hapo hapo Mbezi Beach katika duka hilo.
“Mahitaji ya huduma kwa  wateja sasa ni makubwa na watanzania wanahitaji kupata kile watakachokifurahia katika maisha yao ya kila siku. Hivyo Vodacom kupitia duka hilo itawawezesha wakazi wa Mbezi na maeneo mengine kuwa karibu na upatikanaji wa huduma na kuacha kwenda mbali kama walivyokuwa wakifanya apo awali” Alisema Saleh
Akiongezea kuwa “Bado tutaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu kwa kuzidi kufungua maduka mengi zaidi sehemu mbalimbali ambazo hazijafikiwa na kuhakikisha wateja wetu wote wanaendelea kufurahia huduma zetu za Vodacom, hatimaye kuendelea kubaki kinara kwa kuwapa huduma bora wateja wetu”
Hadi sasa Vodacom inamiliki maduka 72 yaliyo katika sehemu mbalimbali za nchi ambayo yanaendelea kutoa huduma bora na zinazostahili kwa wateja wake kitendo ambacho kinawafanya kuwa ni kampuni inayoongoza hapa nchini.
Upanuzi huu wa wigo wa huduma za mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji kwenye mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mwisho…

mabeste sipo tena B'HITS

(News UPDATE) Kisa cha MABESTE kutoka B'HITZ MUSIC GROUP ni hiki hapa



Baada ya kutamka kuwa hayupo tena kwenye team ya B'hits msanii wa Hip Hop nchini aliwaacha mashabiki wake midomo wazi na wengine kutaka kujua ni nini kimetokea sasa Mabeste amefunguka hapa na kusema
"Tatizo ni maelewano ya kibiashara kati ya mimi na uwongozi wa B"hits na si vinginevyo.....!! Akuna mtu ambaye apendi kuona faida kwenye kazi yake...!! Na kwasababu music ni kazi ...Baaasi nimejaribu kutetea kazi yangu...!! Pamoja saana"

kuwa mzalendo kama J.K Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania (UHURU MARATHON 8 december 2013)

Wednesday, November 20, 2013

Mindu jr.... The future...: Tanzania's Entertainment Blog: (Audio) SQUIZER ft BELLE 9 - MTEMI PESA

Jamafric.blogspot.com: Tanzania's Entertainment Blog: (Audio) SQUIZER ft BELLE 9 - MTEMI PESA

Mindu jr.... The future...: Tanzania's Entertainment Blog: (New Audio) Darasa ft. Mchizi Mox & Shilole - MIKONO JUU

jamafric.blogspot.com: Tanzania's Entertainment Blog: (New Audio) Darasa ft. Mchizi Mox & Shilole - MIKONO JUU

Tanzania's Entertainment Blog: (New Audio) Abby Skills ft. Ally Kiba & Shetta - Basi Njoo Kariakoo


Tanzania's Entertainment Blog: (New Audio) Abby Skills ft. A
lly Kiba & Shetta - Basi Njoo Kariakoo

(Photo) Behind the Camera Last Night DIAMOND ft DAVIDO "NUMBER ONE REMIX"

 

 
Naamini ipo siku nasi Tanzania tutasimama Vyema Katika ramani hii ya muziki Worldwide na kuipa sifa na Heshima zaidi East Africa yetu.... Eeeh Mwenyez Mungu ibariki Tanzania, ibariki East Africa na Africa yetu kwa ujumla.... #LastNight #Onset #NumberOneRemix #DiamondFtDavido #ClarencePeterBehindTheCamera

 Meneja wa Tip Top Babu Tale akiwa na Davido wakati wa utengenezaji wa video hiyo ya Diamond pande za Lekki-Ikoyi (Lekkoyi) Bridge Lagos

diamond awaonesha nigeria kuwa ni bora kuliko wao katika harusi ya PETER

http://www.youtube.com/feature=player_embedded

(Picture) DIAMOND haudhuria harusi ya PETER wa PSQUARE muda huu huko LAGOS-NIGERIA


 

 Pichani ni Diamond Platnumz msanii kutoka bongo akiwa na bwana harusi Peter wa Psquare pale walipokutana huko Lagos Nigeria kwenye harusi ya Peter. Diamond yupo nchini Naija kwaajili ya utengenezaji wa video yake mpya ya wimbo Number One remix aliyomshirikisha msanii kutoka huko huko Naija anaitwa Davido. Nadhani tutegemee mambo mazuri sana kutoka kwa Diamond
 Emanuel Adebayo & Diamond

 Diamond & Iyanya

 Peter & Emanuel Adebayo

 Baada ya hapo ikafika zamu ya Diamond kuwaonyesha wa Naija kuwa na sisi wabongo hayo mambo tunayaweza.

jivunie kuwa wewe

#more

(News) Dar, Pwani wakabidhiwa bodaboda zao

 



 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Hellen Kilawe akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika promosheni ya Timka na Boda Boda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bw.Shadrack Moses  Pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Bw.Matina Nkurlu wakihakiki kadi  ya pikipiki wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Stoo za ofisi hiyo zilizoko Shekilango jijini Dar es Salaam. Pikipiki 25na fedha taslimu zilikabidhiwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Bw.Joseph Mambo akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfungia kamba ya kofia ngumu”Helmet”Mshindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda Bw.Joseph Mambo, Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao.anaeshuhudia kushoto ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

 Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipanda kwenye pikipiki yake aliyoshinda katika promosheni hiyo huku akisaidiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kulia)wakati wa Hafla  ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipunga mkono wakati akiondoka na pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kushoto)wakati wa Hafla  ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

·        Washindi 25 wa Timka na Boda Boda.
·        Washindi 12 walamba Milion kumi na sita
·        Neema zaidi kuendelea kumiminika.
Dar es Salaam, 19th Novemba, 2013….Baada ya washindi zaidi ya 125 kujishindia Boda Boda na wengine kuendelea kujishindia fedha taslimu kila siku kutoka kampuni ya simu ya Vodacom ambazo ni zaidi ya milioni 430 zilizotengwa ndani ya siku 100. Vodacom Tanzania kwa mara nyingine tena  katika kuhakikisha inabadili maisha ya kila mteja wake imekabidhi Boda Boda kwa washindi 25 ambao ni wakazi wa mkoa Dar Es Salaam na Pwani.
Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewashauri watanzania wote kuzidi kuendelea kushiriki katika promosheni hiyo inayoendelea kwa kasi zaidi ya miezi mitatu. Aliendelea na kusisitiza kuwa Kampuni yake imejidhatiti kuhakikisha haipo mbali na wateja wake kwa kuendelea kuwanufaisha kwa kuwapa Boda Boda ambazo zitakuwa ni si tu kuwasaidia kwa usafiri bali  ni msingi mzuri katika kuendeleza biashara zao.
”Kampuni yetu ipo kumnufaisha kila mmoja na imepania vikali kuhakikisha kila mtanzania anapata msingi ambao anaweza kutumia katika kuendeleza biashara zao, kwani siku hizi biashara ya Boda Boda imekuwa ni mwokozi kwa walio wengi ambao huongeza kipato chao kupitia biashara hiyo na ndio maana sisi Vodacom tumetenga piki piki zenye gharama ya kitanzania shilingi bilioni 1 kwaajili ya wateja wetu wote nchini” alisema Matina
Akiongezea kuwa “Kila mmoja anatamani kuwa na msingi ambao utamuwezesha aweze kuwa na biashara yake ambayo itamuingizia kipato matokeo yake kujikwamua katika hali ya kiuchumi, hivyo basi ni wakati wa kila mmoja kunufaika na promosheni mbali mbali zinazazotolewa na kampuni yetu, na ningependa kuendelea kuwashauri wateja wote wanaoshiriki na wanaoanza kushiriki kuzidi kuendelea kwani ni haki ya kila mtanzania kujishindia boda boda kutoka Vodacom”
Ili kuweza kuwa mmoja kati ya washindi kutoka promosheni hiyo ya Timka na Boda Boda ni rahisi sana, wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kushiriki kwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda namba 15544.

(News) Mini ZIFF na Filamu za Bongo in zanzibar


 

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake  (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
  Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
 
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena

(News) KCB TANZANIA YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MKOA WA ARUSHA



 Baadhi ya wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanya kazi wa Benki ya KCB Tanzania,mara baada ya kumaliza semina ya kuelimisha wajasiriamali wa mkoa huo jinsi ya kufanya biashara na kutumia mikopo kwa usahihi,Semina hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo imefanyika kwa siku moja jijini Arusha.

 Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali wadogo na wakati wa benki ya KCB Tanzania tawi la Arusha,Bw.Juma Abdul akitoa mada katika semina ya wajasiriamali wadogowadogo na wakati yenye lengo la kuwaelimisha wajasiriamali wa mkoa huo jinsi ya kufanya biashara na kutumia mikopo kwa usahihi,Semina hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo imefanyika kwa siku moja jijini Arusha.

 Baadhi ya wajasiriliamali wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya wajasiriamali wadogo na wakati wa mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na benki ya KCB Tanzania kwa ajili ya kujifunza jinsi ya kufanya biashara na kutumia mikopo kwa usahihi,Semina hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo imefanyika kwa siku moja jijini humo.

 Mmoja wa wajasiriamali Anna Mrema akipokea cheti chake toka kwa  Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali wadogo na wakati wa benki ya KCB Tanzania tawi la Arusha,Bw.Juma Abdul mara baada ya kufuzu mafunzo ya ujasiriamali wakati wa semina ya wajasiriamali wadogowadogo na wakati iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwaelimisha wajasiriamali wa mkoa huo jinsi ya kufanya biashara na kutumia mikopo kwa usahihi.

Bw.Robert John(kushoto)mmoja wa wajasiriamali wa mkoa wa Arusha akipokea cheti chake toka kwa  Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali wadogo na wakati wa benki ya KCB Tanzania tawi la Arusha,Bw.Juma Abdul(kulia) mara baada ya kufuzu mafunzo ya ujasiriamali wakati wa semina ya wajasiriamali wadogowadogo na wakati iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwaelimisha wajasiriamali wa mkoa huo jinsi ya kufanya biashara na kutumia mikopo kwa usahihi.
by mindu jr..... The future....

Mmwalimu Nyerere na Taifa TANZANIA katika RUSHWA na MUUNGANO

Mwalimu Nyerere aliona mbali
mwalimu nyerere
14 OKTOBA 1999, Tanzania, Afrika na dunia nzima ilipatwa mshituko baada ya kutangaziwa kuwa mwanamapinduzi na mpigania haki na usawa duniani, baba wa taifa la Tanzania, mwanaAfrika mzalendo wa kweli, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameaga dunia huko katika hospitali ya Mt. Thomas, Uingereza alikokuwa akitibiwa.
Leo ni miaka 13 sasa.  Taifa na wapenda haki na uadilifu wote duniani tunamkumbuka.  Alikuwa mwalimu wa kweli.  Mwana wa kweli wa Tanzannia na Afrika.
Tunapomkumbuka, ningependa tujikumbushe mambo mawili aliyoyazungumza panapo Machi 13, 1995 alipokuwa akizungumza na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania.  Mwalimu, pamoja na mambo mengine mengi ya msingi, alizungumzia rushwa na muungano.
Kuhusu rushwa, katika mengi aliyoyazungumza, pia alisema;
‎"Serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi tu basi. Hili jambo ni sheria kama ile ya kwanza niliyowaambiwni kuhusu ubaguzi, mkianza ubaguzi, mtaendelea moja kwa moja; hamna mahali pa kusema simama hapa. Mkisha kuwa wala rushwa, mtaabudu wenye mali. Mimi ni Mkristu, sijui Kuruani inasema nini, lakini msahafu wa Kikristo, Injili, ambayo na Waislamu wanamkubali Nabii Issa, kwa maneno yake mwenyewe "huwezi kutumikia mabwana wawili, mmoja fedha, mwingine Mungu; haiwezekani, utachagua katika wawili hao".
Akazungumza pia kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao umekumbwa na misukosuko kadhaa wa kadha kutoka kwa watu wasioitakia mema nchi yetu.  Mwalimu Nyerere akazungumza mambo mengi sana, kati ya hayo, akasema;
‎"Watu wazima wamezungumza Muungano, kwamba tuuvunje au tuendelee. Ilikuwa ipo hatari ya kuvunjika na wala haijaisha. Watu wamezungumza Uzanzibari, na baadhi ni viongozi wetu, wanajivunia Uzanzibari. Nadhani wengine wanafikiria hata kujitenga. Wapo si wengi; lakini wapo. Kujitenga maana yake ni kuvunja nchi ivunjike tusiwe na nchi moja, tuwe na nchi mbili. Ni jambo linalozungumzwa. Tunataka kiongozi na viongozi watakaoelewa hivyo. Huku kuzungumza Uzanzibari si fahari. Si jambo la fahari. Hatima yake tutavunja nchi. Zanzibar, mtu mwenye akili hawezi kufikiri Uzanzibari ni fahari: hana akili.

Hawezi akautukuza Uzanzibari kwa kujiita 'sisi Wazanzibari' na 'wao Watanganyika'.

Nadhani ile ina usalama ndani yake. Kwamba Uzanzibari ule, Utanganyika ule una usalama ndani yake. Hatima yake Zanzibar itajitenga. Zanzibar ikijitenga kutokana na ulevi tu; sisi Wazanzibari na wao Watanganyika wakumbuke kwamba Muungano ndio unaowafanya wanasema 'sisi Wazanzibari' 'wao Watanganyika'. Nje ya Muungano, hawawezi kusema hivyo: kuna 'wao Wapemba' na 'sisi Waunguja'.

Nataka mjue hivyo. Nje ya Muungano hakuna 'sisi Wazanzibari' 'wao Watanganyika'. Hakuna. Kinachowafanya mjiite 'sisi' ni ubaguzi wa kuwabagua Watanganyika. Wakiisha kuwabagua Watanzania Watanganyika, ile dhambi ya ubaguzi, haifi inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukisha kuitenda inaendelea: ni kama ukila nyama ya mtu utaendelea kuila. Mtamaliza mtatengana na Watanganyika halafu, mara mtakuta kumbe 'sisi' 'si Wazanzibari'. Kuna 'Wapemba' na 'Waunguja'. Wapemba watapata msukosuko kidogo aaolololo!

Mtakuta kumbe kuna Wazanzibari na Wazanzibara! Hamtakaa salama. Hamwezi mkakaa salama baada ya kutenda dhambi ya kuwabagua watu wa nchi yenu ile ile moja mkawaita 'wale wao' na 'hao sii'. Dhambi ile haiishii hapo. Ndivyo historia ilivyo; ni sheria ya historia siyo sheria ya Mwalimu Nyerere. Huwezi kufanya ubaguzi wa namna hiyo halafu dhambi ile ikuache hapo hapo. Hapana itakuandama."
Hivyo ndivyo ninavyomkumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1922-1999) kwa siku ya leo.
Tafakari!
Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani.  Amina.
 
ibrahim mindu
by Mindu jr.... The future

Tuesday, November 19, 2013

Kwa nini nchi za Afrika zinaihara ICC?

MASHIRIKA ya habari yana ripoti juu ya kile kinachoendelea jijini Adis Ababa, Ethiopia kunakofanyika mkutano wa Umoja wa Afrika (AU).  Wakati mkutano huo ukiendelea, Kenya na Sudan zinasemekana kuwa katika mstari wa mbele kuzishawishi nchi zingine za Kiafrika kuisusia Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Hatua hiyo inafuatia kesi kabambe iliyopo ICC ambapo rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta pamwe makamu wake William Ruto wanatuhumiwa kwa kusababisha vurug za uchaguzi wa Kenya mwaka 2007.  Kumekuwa na jitihada za makusudi kutoka ndani ya Kenya, hususani kwa wabunge wa Jubilee wakitaka Kenya kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo.

Jitihada hizo zimetua rasmi jijini Adis Ababa ambapo chombo kikubwa zaidi barani Afrika kinaketi.  Sote tunafahamu kwa nini ni Kenya na Sudan walio mstari wa mbele kushawishi nchi 34 za Kiafrika zilizotia saini Mkataba wa Roma kuisusia ICC.  Wakati rais wa Kenya na makamu wake wakiwa na kesi, naye rais wa Sudan, Omar al-Bashir alishatolewa hati ya kukamatwa kwake.  Ndiyo sababu iliyoifanya hata Marekani kumnyima viza ya kuingia nchini humo kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa majuma machache yaliyopita.

Balozi wa Sudan huko Adis Ababa, bwana Abdul-Rahman Siralkhatim amenukuliwa jana akidai kuwa kitendo hicho cha viongozi wa Kiafrika kinatarajiwa kuwa cha kihistoria zaidi dhidi ya ukandamizaji unaofanywa na mataifa ya Magharibi kwa nchi za Kiafrika.

Kwa nini nchi za Kiafrika haziitaki ICC?  Ni kwa sababu ya ukandamizaji wa Kimagharibi dhidi ya nchi zetu za Kiafrika?  Kwa mtazamo wangu, sababu ni zaidi ya hiyo.  Kama tatizo ni ukandamizaji wa mataifa ya Kimagharibi, hapana shaka nchi za Kiafrika zingekuwa mstari wa mbele kusimama imara kwa pamoja kupinga ukandamizaji wa kiuchumi unaofanya na wawekezaji wa mataifa ya Ulaya na Asia.

Hizi nchi zinazosema mataifa ya Magharibi yanatukandamiza Waafrika kwa kupitia ICC ndizo zilizo mstari wa kwanza kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwa makampuni makubwa ya Magharibi yanayokuja kwa mwamvuli wa uwekezaji huku yakikwangua pasi huruma rasilimali zote za Afrika.  Busara kubwa kwa nchi za Afrika, bara lenye wakazi zaidi ya bilioni moja ikiwa ni zaidi ya asilimia 15 ya idadi ya watu ulimwenguni, ingekuwa ni kwa nchi hizi kuikata mirija ya unyonyaji kutoka kwa mataifa tajiri duniani.  Hili lingewezekana kwa nchi za Kiafrika kuungana pamoja katika kuzisimamia vema rasilimali zilizopo.  Kama nchi ya China imefanikiwa ikijivunia idadi yake ya watu, nchi za Afrika zinashindwa nini?

Leo hii, nchi za Kiafrika zinaiona ICC kama adui yao mkubwa kwa kuwa tu imewagusa wakubwa wenzao.  Lakini tujiulize swali la msingi.  Si kweli ukatili dhidi ya binadamu ulitokea Kenya ama Sudan?  ICC inaweza ikawa na matatizo yake ya kimfumo na utendaji wa kazi.  Tunarejea kwenye busara ya kisheria, makosa mawili hayalihalalishi kosa la pili.

Nchi za Kiafrika zinatambua vema juu ya Wakenya zaidi ya 1000 waliopoteza maisha kufuatia vurugu zile.  Zinafahamu vema juu ya wengine zaidi ya laki sita waliopoteza makazi yao.  Si hilo tu, zinafahamu vema juu ya ripoti ya kurasa 529 ya Tume ya Waki iliyoundwa kuchunguza kiini na wasababishi wa kadhia ile mbaya kabisa katika historia ya taifa hilo la Afrika Mashariki.  Bila shaka pia, nchi hizi za Kiafrika zinakumbuka vema namna mwendesha mashtaka wa ICC wa wakati huo Luis Moreno-Ocampo alivyozipa mamlaka za Kenya mwaka mmoja ili ziweze kuunda chombo cha ndani cha kuwahukumu watuhumiwa hao.  Kenya ikapuuza kufanya hivyo.

Leo hii, jijini Adis Ababa, viongozi wetu wanatuambia mambo ya Afrika yatasimamiwa na Waafrika wenyewe.  Tunajifunza nini kwa mfano huu wa Kenya ilipopewa mwaka mmoja wa kuunda mahakama ya ndani nayo ikapuuza kufanya hivyo?  Tunawaza nini kujisahaulisha kuwa hatua ya ICC kuwafungulia kesi Uhuru na wenzake ilitokana nasi Waafrika wenyewe kupuuza agizo la kujihukumu wenyewe?

Endapo nchi za Afrika zitajitoa kwenye Mkataba wa Roma na hivyo kuamua kutoipa ushirikiano ICC, litakuwa pigo kubwa mno kwa Waafrika.  Hatua hiyo itafungua milango kwa ukandamizaji dhidi ya haki za kibinadamu.  Itafungua milango kwa matukio mengi ya ukatili dhidi ya binadamu huku viongozi wa Afrika wakijivunia kutowajibika pahala popote katika ngazi ya kimataifa.

Wasiwasi wangu ungalipo.  Kiongozi anapoukataa mfumo wa kisheria unaomsimamia namna afanyavyo kazi zake, hapana shaka anataka kuwa juu ya sheria.  Madhara ya kuwa na viongozi walio juu ya sheria ni makubwa mno kwa watawaliwa ambao kwa kawaida ni watu wa chini wasio na nguvu yoyote nje ya sheria kuuondoa ukandamizaji wowote dhidi yao.

Hatua hii ya viongozi wa Afrika inapaswa kutazamwa kwa jicho la usaliti dhidi ya Waafrika wenzao.  Inapaswa kueleweka kama hatua inayokusudia kupiga mhuri wa moto kwenye mamlaka zisizo na kikomo kwa viongozi wa Afrika.

Kama sivyo, kwa nini nchi za Afrika zinaihara ICC?
ibrahim mindu
by mindu jr.... The future

Friday, August 16, 2013

HARAKATI ZA UKOMBOZI ZA AWAMU YA TATU YA UKOMBOZI WA TANZANIA/AFRIKA

LENGO: KUKIONDOA KIINI CHA UKOLONI NA UTUMWA TANZANIA/AFRIKA
NYENZO: ELIMU YA UZALENDO WA WATANZANIA/AFRIKA (ELIMU MPYA)


 Hakuchoka aliendea kuwahamasisha wananchi juu ya kuulinda uhuru watakaoupata............
 hamasa hii ilikua ni kama sala/maombi ambayo yalifanya usafiri huu wa kuliendea taifa jipya uwe kama basi kwa wananchi na viongozi kwenda pamoja bila matabaka.......
 MATOKEO:
 Mwaka mmoja baadae
 Ikabidi kuulizwa viongozi na matokeo ya majibu ya kuridhisha yaliyotakiwa kukosekana......
 Je Sababu ya viongozi kujipangia hayo ni nini?
 DIPLOMASIA? Ikawaje kwa wananchi, Taasisi ya siasa ya umma na Tanzania yenyewe?
 Ndiomana ya haya kutokea....
 Sasa yakafanyika mabadiliko  baada ya kugundulika hiki..




  Endelea kuitembelea blog hii (jamafric.blogspot.com) kujua ukoloni huu mamboleo unawezaje kuondolewa hapa nchini na kutuwezesha kuweza kulifikia taifa la ahadi lililowekwa na waasisi wa uhuru wetu wa mwaka 1961, 1964 na 1967...natumai umepata mwanga ila jua kwamba nyenzo moja ya kukiondoa hiki ni kupata ELIMU YA UZALENDO  kuhusu Tanzania na kuweza kukiondoa kiini hiki...
                                                                                               MGUNDUZI: Bw. Jumanne A. Mindu
                                                                                               MUAANDAAJI: Ibrahim S. Mindu