Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen
Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza
kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa
kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo
visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake
aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa
madawati.
Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi
Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati
ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango
maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya
madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa
tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiria mali hao wakati
wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati
hayo.
Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa
kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu.
Kwa
upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu
kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa
shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea
kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi wilayani
Mtwara.
Mbali na kukabidhi
madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na
kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in
mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.
Ziara hiyo ya mrembo huyo
aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za
kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji
maalumu na yale yasiyopewa kipaumbele.
Mwinzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha
shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika
manispaa ya Mtwara.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment