image in blog

image in blog
mindu

Friday, January 31, 2014

UTALII WA NDANI WA TANZANIA NI WA WATANZANIA WENYEWE

Watalii wa ndani wakifurahia utalii wa kutembea kwa miguu katika hifadhi ya taifa ya Arusha jirani kabisa na kundi la nyati. “PAMOJA na kusikia wakitangaza hifadhi za taifa tulizonazo, huu ni muda muafaka kwa wananchi na watu mashuhuri nchini wakiwemo wanahabari kuzitembelea ili kukuza utalii wa ndani,” anasema Ofisa Mahusiano Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Catherine Mbena. Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utalii wa Tanapa, Dk Ezekiel Dembe anasema lengo ni kufikisha watalii milioni 2.5 ifikapo mwaka 2015. “Tunataka utalii katika hifadhi zetu ukue kwa kuzingatia ubora sio ukubwa ili kulinda ikolojia ya maeneo yaliyohifadhiwa,” Dk Dembe anasema. Hifadhi hizo ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Tarangire, Manyara, Arusha, Mkomazi, Mikumi, Ruaha, Katavi, Kitulo, Udzungwa na vivutio vingine vingi. Mbali na uoto wa asili uliopo katika hifadhi hizo, kuna aina mbalimbali za wanyama kama Simba, Tembo, Twiga, Nyati, Chui na makundi makubwa ya pundamilia, twiga na nyumbu. Kimsingi, umashuhuri wa watu hupimwa kutokana na yale wanayofanya katika jamii, idadi ya watu wanaowaunga mkono, na wengine wanaotaka kuwasikia, kuwasoma, kuwatazama au kufanya mazuri wanayofanya, Mbena anasema. Kitendo hicho huwafanya watengeneze masoko kwa sababu ya kukubalika kwao na kuifanya jamii ichague au ipende kufanya mazuri wanayoyafanya. Mbena anawataja baadhi ya watu mashuhuri wanaoweza kusaidia kukuza utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio tulivyonavyo kuwa ni pamoja na viongozi wa Serikali, dini, taasisi za umma na zisizo za kiserikali; wana siasa, michezo, muziki, waigizaji, wanahabari na wengine wengi. Anasema watu mashuhuri wana maslahi fulani kwa umma na huongoza kwa muonekano kwenye vyombo vya habari ambavyo ni daraja la mawasiliano kati yao na wananchi wengine. Utafiti uliofanywa nchini Australia na taasisi ya Future Foundation mwaka 2007 unaonesha kwamba asilimia 55 ya wanawake na asilimia 39 ya wanaume wanapenda kusikia na baadhi yao kuiga mazuri yanayofanywa na watu mashuhuri. “Kwa mfano wapo Watanzania wamepanda mlima Kilimanjaro baada ya kusikia msanii maarufu wa Bongo Fleva, Lady Jay D kapanda mlima huo,” Mbena anasema akidhihirisha jinsi watu mashuhuri wanavyoweza kusaidia kukuza utalii wa ndani kama watatembelea hifadhi mbalimbali nchini. Anasema Watanzania wengine wametembelea hifadhi zetu baada ya kusikia na kuona kwenye vyombo vya habari wasanii wa kundi la wachekeshaji la The Original Comedy wakitembelea baadhi ya hifadhi ikiwemo hifadhi ya pili kwa ukubwa barani Afrika ya Ruaha. Mbena anawataja watu wengine mashuhuri ambao wamesaidia kutangaza hifadhi zetu ndani na nje ya nchi baada ya kutembelea hifadhi hizo kwa nyakati tofauti kuwa ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mrisho Sarakikya. Na kwa upande wa watu mashuhuri kutoka nje ya nchi, Mbena anawataja baadhi yao ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia kutangaza hifadhi zetu kuwa ni pamoja na muigizaji wa sinema za kibabe Arnold Schwarzenegger wa Marekani aliyetembelea hifadhi ya Katavi. Wengine ni aliyekuwa nyota wa klabu ya Manchester United, David Beckham aliyetembelea Hifadhi ya Serengeti. Mwingine ni Muigizaji maarufu kwa jina la Rambo, Silyveter Stallone wa Marekani aliyetembelea Hifadhi ya Udzungwa na zingine za Kaskazini. Naye mmoja wa matajiri wakubwa duniani na mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abromovich alipanda mlima Kilimanjaro katika tukio lililovutia matajiri wengine wengi ambao kwa mujibu wa Ofisa Mahusiano wa Tanapa, Mbena wanatarajia kuja na kufanya utalii katika mlima huo. Mbena anasema kitendo cha Abromovich kupanda mlima huo si tu kwamba kimeamsha ari kwa matajiri wenzake kuja nchini na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo, bali pia kimeamsha hali kwa Watanzania hususani wale ambao ni wapenzi wa klabu ya Chelsea kuupanda mlima huo. Akiwa amevaa jezi inayotumiwa na klabu hiyo, Jackson Mtambalike aliyekutwa na mwandishi wa makala haya nje ya lango la kuingilia katika hifadhi ya mlima huo hivi karibuni alisema “baada ya kusikia Abromovich kapanda mlima huu, niliweka dhamira ya kuwa mmoja wa mashabiki wa Chelsea kupanda mlima huu ili kuunga mkono kilichofanywa na mmiliki wa timu hiyo.” Katika tukio la hivi karibuni, mtoto wa Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton, Chelsea Clinton na Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra kwa nyakati tofauti walitembelea Hifadhi ya Tarangire na Serengeti. Chelsea Clinton alinukuliwa na Jarida la Tanapa Today la mwezi Julai-Septemba, 2013 akiwa Hifadhi ya Tarangire akisema “ Nikiwa hapa Tanzania nimetembelea moja ya hifadhi ambayo asasi ya Wildlife Conservation Society inafanya utafiti wa tembo na kushirikiana na Serikali ya Tanzania kulinda kiumbe hicho.” Chelsea aliyeona tembo mtoto mwenye miezi mitatu akicheza huku mama yake mwenye miaka zaidi ya 30 akionekana kumlinda anasema “hawa ni viumbe wa kuvutia na wasio na hatia, ni muhimu kwetu sote tukawalinda.” Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST), Godwell ole Meinng’ataki anasema Tanzania imekuwa ikipata fedha nyingi kutoka kwa watalii wanaoingia hifadhini kuangalia tembo na wanyama wengine. “Bila shaka kiasi cha fedha wanachopata majangili wa meno ya tembo hakiwezi kuwa sawa na kile kitokanacho na utalii; ni muhimu tembo na wanyama wengine wakaendelea kuwepo kwa faida ya sasa na kizazi kijacho,” anasema. June mwaka huu 2013, Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa naye alitembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na kuvutiwa na mandhari yake nzuri iliyosheheni wanyama mbalimbali. “Haya ni maajabu ya dunia, sijawahi kuona makundi makubwa ya nyumbu na nyati kama niliyoyaona Serengeti; nitawaambia watu wangu na naahidi kurudi tena na tena nikiwa na familia yangu,” anasema. Muongoza watalii wa mjini Arusha, Jackson Mollel anasema kwa miaka mingi watangazaji wamewatumia watu mashuhuri kutangaza bidhaa zao na kuongeza masoko ya huduma au bidhaa zao. Tunataka watu mashuhuri wa ndani ya nchi watembelee hifadhi zetu, hii itahamasisha Watanzania wengine kutembelea na hatimaye kuinua utalii wa ndani, Mollel anasema. Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utalii wa Tanapa, Dk Dembe anasema wakiwa katika lengo la kupokea watalii milioni 2.5 ifikapo 2015, idadi ya watalii wa ndani na nje inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Lengo la Tanapa lilikuwa kupokea wageni milioni moja ilipofika mwaka 2010, lakini hadi sasa hifadhi zetu zinapokea watalii wanaokaribia milioni 1.5 huku zaidi ya asilimia 90 wakiwa ni wale wanaotoka nje ya nchi. Anasema lengo la kupokea wageni milioni 2.5 linatakiwa liende sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya barabara ndani ya hifadhi, viwanja vya ndege na huduma kwa wageni. “Zipo huduma za waongoza watalii na usafiri, malazi na vyakula ndani na nje ya hifadhi, vyote kwa pamoja ni lazima viendelee kuboreshwa ili viendane na mahitaji tofauti ya watalii,” anasema. Dk Dembe anasema katika kuboresha huduma kwa watalii tunataka “waongoza watalii na madereva wazingatie taratibu za hifadhi; tutawapa mafunzo madereva wote wanaoingia hifadhini.” Anasema madereva hao watapewa vitambulisho na endapo watakiuka taratibu za hifadhi watanyang’anywa vitambulisho vyao na kuzuiwa kubeba watalii hifadhini kwa usalama wa vivutio ndani ya hifadhi na watalii wenyewe. Anasema safari na utalii ni vitu vinavyokwenda pamoja hivyo ni muhimu kwa wadau wakaboresha sekta ya usafiri na kutoza gharama kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi hasa kwa Mtanzania wa kawaida. “Kwa upande wetu tunaendelea kuimarisha mtandao wa barabara ndani ya hifadhi na lengo letu ni kuona barabara hizo zinajengwa kwa kiwango ambacho zitapitika kwa mwaka mzima,” anasema. Kwa upande mwingine Serikali ya Rais Kikwete nayo inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nje ya hifadhi ambazo nyingi zinajengwa kwa kiwango cha lami.Kuhusu huduma ya usafiri wa anga, Dk Dembe anasema mbali na hifadhi za Kaskazini kuwa na kiwango cha kuridhisha, kukamilika kwa uwanja wa Songwe Mbeya na baadhi ya kampuni za ndege kuanzisha safari kwa kutumia viwanja vya mikoa kutaboresha huduma hiyo kwa mikoa ya Kusini. Katika kuinua utalii wa ndani, Martin Jones ambaye ni mtalii kutoka Australia aliyetembelea Hifadhi ya Serengeti hivi karibuni anasema “huduma ya usafiri haipaswi kuwa kikwazo kwa Watanzania.” “Kuna kampuni za usafiri wa watalii zinatoza kwa siku Dola za Kimarekani 250 (sawa na zaidi ya Sh 400,000) kwa mtalii mmoja; kiasi hicho ni kikubwa kwa watalii wa nje lakini ni kikwazo kwa watalii wa ndani,” anasema. Naye Lizy Stewart mtalii kutoka Uingereza aliyetembelea Hifadhi ya Tarangire hivi karibuni anasema sekta ya usafiri inatakiwa iwe sekta ya huduma ikiwa ni ‘sehemu ya uchumi wa taifa inayohudumia msafiri anayetembelea eneo nje ya eneo analokaa au kufanya kazi.’ Mkurugenzi wa Kampuni ya Tatanca Tours ya mjini Iringa, Denis Ngede anasema “kuongezeka kwa watalii wa ndani kutasaidia kupunguza gharama za uendeshaji ambazo kwa asilimia kubwa hutegemea watalii kutoka nje na hivyo kupungua kwa gharama za safari.” Mmoja wa watalii wa ndani aliyetembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire, Arusha, Manyara na Mlima Kilimanjaro, Tukuswiga Mwaisumbe anasema “nimeandika historia katika maisha yangu.” Mwaisumbe (40) anasema katika historia ya maisha yake hakuwahi kufikiria kutembelea hifadhi hizo akihofia gharama kubwa. “Kwa Mtanzania wa kawaida ni ngumu kutembelea hifadhi hata kwa siku moja akiwa peke yake; kitakachomuongezea gharama ni usafiri wa kukodi, lakini wakiwa katika makundi ni rahisi kutembelea hifadhi kwani gharama itakuwa ya kuchangia,” anasema. Akitoa mfano, Ofisa Utalii wa Tanapa wa Ofisi ya Utalii ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Risala Kabongo anasema gharama ya kukodi Coaster yenye uwezo wa kupakia watu 25 kutoka Iringa Mjini hadi Hifadhi ya Ruaha ni Sh 500,000. “Kiasi hicho kinamfanya kila mtu achanngie Sh 20,000 ambayo kimsingi ni nafuu sana ikilinganishwa na Sh 500,000 anazoweza kulipa mtu mmoja kwa kukodi Toyota Land Cruiser kwa siku moja,” anasema. Akizungumzia gharama za kuingia hifadhini, Kabongo anasema ni kati ya Sh 1,000 na Sh 15,000 kwa mtu; gharama hiyo ikizingatia makundi ya wanafunzi, watoto na watu wazima. Kuhusu huduma za malazi na vyakula, Dk Dembe anasema Kanda ya Kaskazini inazidi kupiga hatua kubwa na kwamba mkakati wao ni kuwashirikisha wadau kuboresha sekta hiyo katika Kanda ya Kusini. “Tunahamasisha wafanyabiashara waanzishe kampuni za utalii katika mikoa ya Kusini; lakini pia tutafanya makongamano ya uwekezaji Februari mwakani,” anasema. Kwa kupitia makongamano hayo, Tanapa itatangaza kuuza maeneo ya uwekezaji wa hoteli za kitalii katika hifadhi zake na watakaopata maeneo hayo watatakiwa kuanza kuwekeza katika kipindi cha miezi sita. Katika mchakato wa kuifanya sekta ya utalii iendane na wakati, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki hivi karibuni alinukuliwa akiahidi kwamba Serikali itazifanyia marekebisho sheria, sera na kanuni zinazohusu sekta ya utalii ili ziendane na wakati. Alikuwa akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge pamoja na wawakilishi wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato) kwenye semina ya kujadili changamoto na faida ya sekta ya utalii. Kagasheki anasema sheria, sera na kanuni zinazoongoza sekta ya utalii zilizopo zimepitwa na wakati na zimekuwa zikichangia kudorora kwa sekta hiyo ikiwemo kuwavutia wawekezaji. Alisema wawekezaji hukatishwa tamaa na milolongo ya kupata vibali husika, hivyo huamua kukimbilia nchi jirani ambazo sasa zinapiga hatua nzuri katika utalii. “Wenzetu wa Rwanda mwekezaji anapotaka kuwekeza katika sekta hiyo hupewa vibali kwa siku zisizopungua saba, sisi hapa kwetu huchukua zaidi ya mwaka mmoja, urasimu huu ndiyo unaotumaliza,” anasema. Kuhusu usalama wa watalii wawapo hifadhini, Dk Dembe anasema kikosi cha Polisi wa watalii kimeanzishwa na kwa kushirikiana na polisi jamii kitahakikisha watalii wanakuwa salama katika kipindi chote wanachotembelea hifadhi. Kwa mujibu wa tafsiri ya Kimataifa na ile ya Shirika la Utalii Duniani, mtalii ni mtu yoyote yule aneyesafiri kutoka katika maskani yake ya kawaida na kwenda sehemu nyingine na kukaa huko kwa zaidi ya saa 24 kwa madhumuni tofauti.

(News) MILLEN HAPPINESS MAGESE ATEMBELEA MAENDELEO YA MIRADI MTWARA



Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati.

Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiria mali hao wakati wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.


Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu.
Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi wilayani Mtwara.


Mbali na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.


Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa kipaumbele.


Mwinzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika manispaa ya Mtwara.

Mwisho.

RAISI KIKWETE AKIMUAPISHA.................................

leo Jan 30, 2014. Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,

Thursday, January 30, 2014

Picha na Taarifa Rasmi:Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye Azungumza na Waandishi wa Habari Leo Nakusema Miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kinajivunia Sana Mafanikio Waliyoyapata Ambayo ni :-
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano CCM Mbeya.Picha Adam H. Mzee Ccm Yajivunia Mafanikio Waliyopata
Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Bunge:Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda anatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) --
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda (Mb) anatarajia kurejea nchini siku ya Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 akitokea Geneva, Uswisi alikoenda kuhudhuria mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Maspika Duniani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015. Kamati hiyo inayoundwa na Maspika 37 walioteuliwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) imekutana tarehe 27 – 28 Januari 2014 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mabunge Duniani Mjini Geneva. Mkutano wa pili wa Kamati hiyo ya Maandalizi utafanyika mwishoni mwa mwaka huu. Aidha, kabla ya kwenda Geneva, Mhe. Spika alihudhuria mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofanyika Wellington, New Zealand kuanzia tarehe 22 hadi 24 Januari 2014. Kwa ujumla, ushiriki wa nchi kwenye Mikutano ya Kimataifa huwa fursa nzuri ya kuitangaza na kuipa heshima nchi yetu. Vile vile Mikutano hiyo huwa jukwaa madhubuti linalotumika kuiweka nchi katika ramani ya dunia na kuonyesha vivutio hususan katika nyanja za uwekezaji, utalii na maliasili pamoja na fursa mbalimbali zilizomo. Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, DAR ES SALAAM 28 Januari 2014

TANZANIA NI NCHI YA KWANZA BARANI AFRIKA KWA SAFARI ZA UTALII , SERENGETI NA RUAHA IRINGA ZAONGOZA

Kaimu mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe ( kulia) akimakabidhi Bi Jane Mwakinyuke kutoka Hifadhi ya Taifa Mikumi , cheti cha kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja ya kuongoza watalii katika hifadhi za Taif
Kaim mkurugenzi mkuu wa TANAPA DR Ezekiel Dembe wa pili kulia waliokaa akiwa na kaim mhifadhi wa Ruaha Bw John Nyamhanga kulia ,Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST kushoto wa pili na kaimu RAS Iringa pamoja na walimu wa mafunzo hayo na askari waliohitimu mafunzo waliosimama
Askari pekee wa kike kutoka hifadhi ya Taifa ya Ruaha Jane Griffin Mwakinyuke ambae amehitimu mafunzo ya kuongoza watalii katika utalii wa miguu hifadhini akionyesha cheti chake
a ambao hupenda utalii wa miguu juzi ambapo jumla ya askari 20 kutoka hifadhi mbali mbali walihitimu mafunzo hayo,kulia kwake ni Bw Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST' Na FRANCIS GODWIN BLOG TANZANIA yazidi kung'ara katika sekta ya utalii barani Afrika baada ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa kwa kuvutia zaidi watalii katika safari za utalii katika hifadhi hiyo huku hifadhi ya Serengeti na Ruaha Iringa zikiongoza kwa ubora ya utalii. Kaim mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja ya kwa askari 20 ,mafunzo ya utalii wa miguu katika hifadhi hiyo ya Ruaha na nyingine kama Mikumi na Udzungwa yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa . Dr Dembe alisema kuwa Tanzania imeonekana ni nchi ya kwanza kwa utalii baada ya wataalum wa masuala ya utalii barani Afrika kuchagua nchi nane barani Afrika ambazo zinafaa kwa kufanya safari za utalii Alizitaja nchi zilizoshindanishwa kwa kupigiwa kura kuwa ni Tanzania , Botswana , Uganda , Namibia ,Afrika ya kusini , Kenya , Zambia na Zimbabwe na huku Tanzania ikionekana ni nchi inayoongoza kwa safari za kitalii ukilinganisha na nchi nyingine zilizowekwa katika orodha hiyo. Pia alisema mbali ya kuchagua nchi inayofaa kwa utalii pia wataalam hao walitazama maeneo 50 yaliyofaa kwa safari za utalii na Tanzania ikifanikiwa kupata maeneo 10 bora zikiwemo hifadhi 8 ambazo zipo katika TANAPA na Selous na Ngorongoro huku mlima wa Kilimanjaro haukuwekwa kutokana na hifadhi hiyo ya Kilimanjaro ni maalum kwa kupanda mlima pekee. Hata hivyo alisema katika hifadhi hizo 10 bora kwa hifadhi za kusini hifadhi ya Ruaha imeongoza ikifuatiwa na katavi wakati hifadhi ya kwanza kwa hifadhi bora ilikuwa ni Serengeti wakati hifadhi ya pili ilikuwa ni hifadhi ya Ruaha barani Afrika ambazo zilionekana ni bora na vinavutia zaidi kwa safari za kitalii. Dr Dembe alisema kuwa hivi sasa TANAPA wameelekeza nguvu zote katika kuendelea kuitangaza hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kubadilisha mazingira ya hifadhi hiyo ili kuvutia idadi kubwa ya watalii katika hifadhi hiyo ambayo ndio hifadhi kubwa kuliko zote katika Tanzania. Hata hivyo alisema kuwa katika kuboresha utalii wa kusini TANAPA ipo katika mkakati wa kutoa elimu kwa madereva wanaopeleka wageni katika hifadhi mbali mbali ikiwemo hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ili kuona kampuni za kitalii kuwa na madereva ambao wanajua vema utalii na kuepuka udereva wa vurugu katika hifadhi. Alisema kuwa utalii ni sekta nyeti katika Taifa hivyo lazima wale wote wanaohusika na masuala ya utalii kuwa na elimu ya kutosha juu ya utalii na kuyataka makampuni kuepuka kuwatumia madereva wa daladala kupeleka wageni hifadhini ambao baadhi yao wamekuwa hawana elimu ya utalii . Kuhusu askari hao 20 waliopewa mafunzo Dr Dembe aliwataka kuwa wazelendo na hifadhi pamoja na Taifa zima la Tanzania na kuepuka kugeuka kuwa maadui wa hifadhi kwa kushirikiana na majangili kuhujumu hifadhi hizo . Wakati huo huo Dr Gembe alivitaka vyombo vya habari na wanahabari nchini kuendelea kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na kuepuka kuandika habari ambazo hazisaidii katika ukuzaji wa sekta ya utalii . Alisema iwapo vyombo vya habari nchini vitafanya vizuri katika kuhamasisha utalii na kuwa na uzalendo na Taifa la Tanzania katika kuepuka kuandika habari za kutisha wageni kufika katika hifadhi ni wazi sekta ya utalii nchini haitakuwa . Kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ruaha Bw John Nyamhanga mbali ya kuomba TANAPA kusaidia kumaliza kero ya vitendea kazi kwa askari hao bado alisema kuwa mafunzo hayo ya utalii wa miguu kwa askari hao ni mzuri zaidi japo mafunzo hayo yanaweza kukwamisha upande mmoja katika utendaji kazi wa kila siku katika hifadhi hiyo ya Ruaha . Kwani alisema kuwa askari hao ndio ambao wamekuwa wakitumika katika shughuli nyingine za hifadhi hiyo hivyo iwapo TANAPA haita ongeza idadi ya watumishi wengine kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya watumishi wa idara nyingine . Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST alisema kuwa lengo la SPANEST ni kuendelea kuboresha zaidi hifadhi ya Ruaha ni nyingine ili kuwavutia zaidi watalii wa ndani na nje kufika katika hifadhi hizo .

SIKU YA SHERIA KUAZIMISHWA TAR 3TH FEBRUARY

Siku ya sheria yatarajiwa kuazimishwa tarehe 3 mwezi wa pili nchini kote ambako watu wanatakiwa kusheherekea siku hiyo kwa kuzitambua sheria na haki zao ambazo zitawafanya waishi na kujua nini haki na ni ipi inayomfanya binadamu/mtanzania kuwa na amani ya kutembea na kufanya shughuli zake bila ya ghubudha ambayo haistairi, kwani sheria na kufanya shughuli mahali popote nchini ni haki ya kila mtanzania... hivyo tunahitajika kusoma na kujua haki na sheria ambayo itakulinda popote uendako