Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum, ambaue alikuwa mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA, aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ameaga dunia.
Zitto ametoa taarifa hiyo katika kurasa zake za Facebook na T
Rais Jakaya Kikwete alipomjulia hali Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe aliyekuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangilizi maalumu (ICU) katika hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam hivi majuzi. (picha: Freddy Maro/IKULU)
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, bi. Shida alianza kusumbuliwa na maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.
Zitto alinukuliwa akisema kuwa, baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.
Zitto, ingawaje alisema hali ya mama yake haikutengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo, alikuwa na matumaini: “Hali ya mama kwa kweli siyo nzuri, lakini nina imani itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kama zamani,” alisema Kabwe ambaye alidai kuwa kutokana na maradhi hayo ya mama yake, alishindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
P
No comments:
Post a Comment