image in blog

image in blog
mindu

Thursday, February 6, 2014

RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA NI ZAWADI YA MWAKA 2014 YENYE CHANGAMOTO LUKUKI.

Mnamo karne ya 19 baadhi ya wahenga wetu waliopata harufu ya elimu ya uzalendo kupitia moto wa jioni iliyopata harufu ya utu, waliutafuta uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ambazo baadae zimeungana na kujiita Tanzania. kwa kuwa hatukuwa na elimu ya uzalendo ya kutuelimisha tulikotoka, tukadhani muungano wetu umeanzia pale tukaanza kumegana. tumeanza kuiona hatari mbele yetu tumeunda tume ya katiba mpya ituunganishe upya. Baada ya kazi ngumu yenye Majonzi, mnamo tarehe 30/12/2013 Tume ya mabadiliko ya katiba ya Tanzania mmemudu kutukabidhi watanzania wenzenu rasimu ya pili ya katiba mpya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwa Rais wa Zanzibar; Hongereni sana.
Kwa tendo hili kufanyika ukingoni mwa mwaka 2013. Tunaweza kuichukulia kama zawadi ya kuingia nayo mwaka mpya wa 2014. Zawadi hii unaweza kuwa uwanja wa kujiandikia historia, pia inaweza kuwa kurunzi, darubini na uwanja, vitakavyotuwezesha kuona mbali na kuandika dira ya maisha yetu naya vizazi vyetu kwa miaka mingi ijayo. lakini ubora wa zawadi hii unatengemea maoni tutakayoyatoa watanzania wenyewe kwa bunge letu la katiba mpya. Pia umahiri wa wabunge wa bunge la katiba mpya watakao yapokea na kuyajadili maoni yetu pamoja na yaliyoandikwa ndani ya rasimu ya pili ya katiba mpya, hatimae kutupatia mapendekezo ya katiba mpya yatakayo kubaliwa na zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wenye umri na sifa za kupiga kura kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo.
Kwa kuiona kazi ngumu iliyombele yetu ya kuifanya zawadi hii inayogusa maisha ya watanzania wa sasa na wajao iweze kufikia kiwango cha ubora tarajiwa, viongozi wa ngazi mbalimbali kupitia majukwaa mbalimbali waliotoa nasaha kwa wajumbe tarajiwa wa bunge la katiba. Naomba nasaha zile zituhusu pia sisi tutakaokaa nje ya bunge la katiba kwa kutoa maoni ya kulijenga na kuliendeleza taifa letu, pengine tujigeuze makachero na askari dhidi ya matajiri watakaotaka kuwanunua wabunge wa bunge la katiba ili wafanikishe matarajio yao pekee.
Ombi hili kwa watanzania wenzangu linakusudia kujenga zingatio na ushiriki mpana na wakufaa katika jambo hili nyeti kwetu na kwa vizazi vyetu bila ya kuujali mgawanyiko wetu wa namna yoyote ile. Ili dhamira ya ombi hili itimie tunapaswa kujiongezea uwezo wa uelewa juu ya nasaha za viongozi wetu kwa kuyaeleza yale yaliyojificha ndani ya nasaha zile, ambazo baadhi yake ni hizi hapa:-
a) Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania anaasa juu ya makundi na mitazamo yao ndani ya bunge la katiba.Ameasa hivyo kwavile tayali taifa limeshamegeka katika makundi manne au matano makuu, ndani yake mkiwa na vikundi vidogo vidogo (b) Waliosikiliza vyema na kuelewa mjadala nilioufanya na wana habari wa ITV kwenye studio zao tarehe 26/04/2012 na 31/05/2012 watakuwa wamemuelewa vema mheshimiwa Rais. (c ) Mjadala ule umebaini kuwa taifa liko kwenye matabaka makuu manne ambayo yote yataingia kwenye bunge la katiba bila ya kujali ni wanaume, wanawake, walemavu, vijana au wazee. na hayo ni. i. Wanasiasa – humu mna (a) wanasiasa tawala badala ya wanasiasa ongozi na (b)wanasiasa pinzani badala ya wanasiasa shindani. hawa ni waidhinisha ilani, sera na sheria na usimamizi wake piawaendeshaji siasa iliyochaguliwa na taifa kuifuata. ii. Wasomi wa elimu za kawaida na wa kidini – humu hupatikana watawala na watendaji. Hawa ndio wanaotunga/wanaoanda ilani na sera ndani ya vyama vya siasa, watunga/waandaa sheria na uwendeshwaji wake ndani ya serikali. iii. Watu au raia wanaoitwa wa kawaida - kwa sasa humu unawakuta watu wenye shahada ya kwanza wasio na watu wa kundi (i), (ii) na (iv) juu yao, hadi wale wasiosoma elimu za kigeni kabisaHawandio watekelezaji wa yanayoamuliwa na makundi mengine aidha maamuzi hayo yawe mazuri au mabaya kwao; yoyote ya matendo yao maana baadhi yao wamekata tamaa.
iv. Matajiri wa ngazi mbalimbali – baadhi yao wametokea kwenye makundi hayo matatu, wengine wageni wa nchi za nje, haijalishi wao wamo kwenye bunge hilo au la, ila hutumia walichonacho kununua fikra za wajumbe ili matarajio yao yatimie, hawa hawana cha kuopoteza kwa uharibifu wa taifa husika ila maslahi yao tu. d) Katika mgawanyiko huu, alilolihofu mheshimiwa rais ni rahisi kutekelezeka kwa vile taifa hili halijawahi kuwa na elimu ya uzalendo kwavile wakoloni hawakuwa wanafundisha wala kuendesha siasa, hapa, ila makwao. Hapa walifundisha na kuendesha utawala na uraia tu. Kwa bahati mbaya hata wachache waliopata harufu ya uzalendo kutokana na kufundishwa historia yetu halisi kwa kina, mfumo ya siasa japo ilikuwa ya wenzetu, mafunzo ya JKT tulikopeana uchungu wa taifa letu pamoja na hadithi za moto wa jioni wa wazee wetu vijijini. e) Aidha baada ya kuundwa bunge la katiba, kabla ya kuanza kazi kwanza lipewe japo mwanga wa elimu ya uzalendo. Baada ya utafiti wa miaka 25 nimeigundua, nikipewa nafasi naweza kuwafanya wajitambue, walitambue taifa wanalolizungumzia, nafasi yao kwa watanzania wa leo na wajao na uchungu kwa taifa lao. Hapo ndipo tutakapoweza angalau hofu ya Mhe. rais kuwa ngumu kutokea. tarajio kubwa katiba mpya nikuyarudisha pamoja makundi yote ya watanzania yaliyotajwa hapo juu na kuliimarisha taifa letu. lakini kama niliyoyasema tarehe 26/4/2012 kuwa kwenye mgawanyiko huu kuna uwezekano wa kupata.
1. katiba mangimeza itakayoundwa na wanasiasa tawala waendelee kutawala. 2. katiba mapinduzi itakayoundwa na wanasiasa upinzani uweze kushika dola. 3. katiba faulisha au ya kulikiza itakayoundwa na waso,mi ili kulihamisha taifa letu kufikia kuelekea matakwa au mambo ya kule walikopatia elimu ao za juu. 4. katiba ustaarabisho; hii ni katiba itakayoundwa na matajiri kwa kuyatumia makundi ya hapo juu, ili kuwaamisha viongozi wa taifa husika kuwa wao ni bora kuliko wananchi waliowachagua na wenye nchi ili wavune wanavyovitaka. 5. katiba ya kitaifa tunayoitarajia itakayo tukusanya sote, wa makundi yote. Mbali ya mambo mengine, hofu ya mhe. rais inajitokeza tena katika ujenzi wa taifa lenyewe la Tanzania. Tanzania bara wanautaka mfumo wa serikali tatu ili kulifufua au kuirudisha nchi Tanganyika na serikali yake au vyake kwa vile Tanzania visiwani wameirudisha Zanzibar yao na baadhi ya vitu vyake kwenye katiba ya awali. Hapa viongozi wengi wanahofu kuvunjika kwa muungano, kufa kwa CCM na kurudi kwa vyama vya zamani na wengine walihofia uwepo wa Zanzibar nje ya muungano. Hakuna haja ya kuziacha hofu hizi ziungane na kuwa tukio kamili, ni vema kuyawahi kwa kuituma katiba yetu mpya itufanyie yafuatayo:- i. Iturudishie siasa yetu asilia isiyofungamana na upande wowote iliyo ya wote iliyotajwa mwanzoni mwa uhuru wetu badala ya kuitumia kama sera ya uhusiano wa kimataifa tu, kama tatizo maandishi mimi nimeyagundua katika utafiti wangu wa miaka 25 ninao mswada wa hili. ii) Vyama vyote nchini viitumie siasa hii na sera zake, watofautiane katika ilani ya kuimarisha siasa hii na sera zake, hapa tutapata vyama shindani vya siasa. iii) Siasa na sera hizi zitatuzibia nyufakatiba uimarishaji taifa Tanzania zilizopo sasa ambazo ndiyo msingi wa changamoto za muungano za sasa tulizozitengeneza wenyewe kwa kurubuniwa na wageni kupitia nyufa hizi. Hapa tutarejea kuwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichaguliwa bara makamu wake atachaguliwa wa Zanzibar bila ya kujali anatoka chama gani, vyivyo hivyo kwa kinyume chake. iv) Hapa tutaweza kukidhi matakwa ya wengi kwa kuwa na serikali tatu zenye sura ya serikali moja imara ya kitaifa. Kila upande wa Jamhuri ( Tanganyika na Zanzibar ) zote zitakuwa na madaraka ya ndani, zitakuwa na serikali, wimbo wanchi/jimbo kuu, bunge lao, ila zote zifuate siasa na sera za kitaifa, ilani ya chama kilicho shinda itailea siasa na sera ya taifa kwa kipindi hicho; kwa vile vyama vyote vya siasa vitakuwa na sera ya taifa zinazotokana na siasa moja ya taifa sio siasa za kuazima toka ugenini, hivyo haitokera. v) Baadae marais wa Tanganyika na Zanzibar ama ndio watakaopigiwa kura nani awe rais wa jamhuri na aliyebaki awe makamu wake ama kwa zamu ya Tanganyika na Zanzibar kuongoza jamhuri ya muungano kwa kadri bunge la katiba litakavyoona linafaa. Wabunge wa bunge la muungano nao watokee kwa wabunge wa Zanzibar na Watanganyika; hii itapunguza gharama za uendeshaji wa serikali ya aina mpya ya muungano, itakayokuwa na serikari za Tanganyika au Zanzibar. Tuwe na baraza kuu la siasa, ili rais apate ushauri wa kitaifa kwenye mambo mbalimbali. Wengine wanahofia mtindo wa kuwawajibisha mawaziri/viongozi kwenye wizara na kuwaacha watendaji na watekelezaji wanafanya makosa haya moja kwa moja. Hii ni changamoto iliyofanywa na wanasiasa wenyewe ama kwa matumaini Fulani ama kwa kutoka nje ya njia au kuacha mamlaka yao; hali hii ilianzia kwenye vyama vya siasa vyenyewe. Kuliondoa hili ni lazima tuiombe katiba mpya iyandoe mapinduzi ya mamlaka na madalaka yaliofanywa na utawala/serikali dhidi ya uongozi/mamlaka zao toka kwenye vyama vya siasa hadi serikalini na kwa wananchi wao Hapa ndipo inapoongeza haja ya kuanza kampeni ya kufundishana elimu hii mpya nchi ambayo ndiyo pekee itakayotufanya tuifakie hadhi ya utu na kututoa kwenye ukoloni mamboleo kutupatia uhuru kamili na kutukinga tusiwe tegemezi na kurudishwa tena kwenye ukoloni au utumwa tena baada ya huu ukoloni mamboleo wa sasa ukikomaa.
Mimi: Bw J. A. Mindu – mtafiti na mgunduzi binafsi wa Falsafa na Elimu ya Uzalendo wetu