image in blog

image in blog
mindu

Thursday, August 21, 2014

AZIMIO: AZIMIO LA ARUSHA NA TANZANIA YETU



AZIMIO LA ARUSHA

AINISHO(MAANA) YA AZIMIO LA ARUSHA
Azimio la arusha ni maamuzi yaliyofanywa na halmashauri kuu za TANU na AFROSHIRAZ  PART huko Arusha Tanzania, yaliyoendana na utekelezaji wa urekebishaji wa taifa letu.



KUUNDWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
Azimio la arusha liliundwa mwaka 1967 kupitia kikao cha mseto wa  Halmashauri hapo juu. Mjini arusha Tanzania.

SABABU YA KUUNDWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
Baada ya kugunduliwa kwa madhumuni, dhima na malengo ya kutafutwa kwa uhuru wetu kwa wananchi wake yamevunjwa. Huenda utawala/serikali wameupindua uongozi, kuutenganisha uongozi na wananchi kiasi kuonekana kama vile serikali imefanya kazi ybila ya uongozi au wananchi juu yake; wakawa kama wakoloni weusi. Hivyo azimio la arusha lilibeba maazimio/maamuzi mengi ya kurekebisha hali hii na kujenga dira ya taifa na ulinzi wake.



MADHUMUNI YA AZIMIO LA ARUSHA
1.      Kujenga miiko, maadili, nidhamu, kanuni na sheria za kudhibiti hali iliyotajwa hapo juu.
2.      Kwa kuwa baada ya uhuru kulionekana kutokuwepo kwa siasa ya kitaifa ya kuimarisha umoja na mshikamano wetu, kulianzishwa na kutangazwa kwa siasa ya kitaifa. Lakini kwa vile wasomi hawakuitafiti siasa ya kutofungamana na upande wowote iliyotajwa wakati wa uhuru mwaka 1961, wakaitafuta siasa inayofanana nayo na yenye vitabu iliyoonekana siasa ya ujamaa na kujitegemea. Wakaitangaza na kuanza kuifata ile ya mashariki japo si lengo.


3.      Walitaja hali ya taifa kwa wakati ule nayo ni:
(i)                 Pamoja na uhuru tulionao lakini bado tupo kwenye ukoloni mamboleo. Kwa bahati mbaya hapakuwa na maelezo zaidi juu ya ulivyo, ulipo na namna ya kuuondoa; wala hakuna aliyeushugulikia tena. Wala haukutajwa uzito au athari za aina yani ukoloni kwetu na kwa uhuru wetu.
(ii)               Azimio lilidai kuwa bado tuna maadui UJINGA (hapa palichukuliwa kuwa ujinga ni kutokua na elimu ya kigeni tu), MARADHI na UMASIKINI.
(iii)             Azimio lilitaja dawa au udhibiti wa maadu hao ni kuwa ungozi bora, siasa safi, watu na ardhi lakini bila ya ufafanuzi wake; ni nini au vipi upatikanaji wake?
(iv)             Paliazimiwa kutoa huduma kwa jamii, kukuza elimu ili kuongeza wataalamu, pia kukuza vipaji  vya wenye ufundi mbalimbali mijini na vijijini. Palitolewa tamko la KILIMO NI UTI WA MGONGO wa uchumi wa taifa letu ili kuongeza ajira.






UTENDAJI WA AZIMIO LA ARUSHA
1.      Palitengeneza miiko ya uongozi iliyozaa maadili, miiko na nidhamu kulikoiondoa hali yote iliyojitokeza awali.


2.      Palitangazwa siasa ya ujamaa na kujitegemea kuwa siasa ya kitaifa. Ikadaiwa uongozi unnashika hatamu ya uongozi, serikali iliwekwa chini ya uongozi wa ngazi zote nchini.

3.      Watu/wananchi waliwekwa pamoja vijijini na huhuma za shule, zahanazi, maduka na kadhalika vilipelekwa karibu yao vijijini na mijini.

4.      Ukuzaji wa vipaji vya ufundi ulianzia vijijini hadi mijini.


5.      Demokrasia iliongezeka kupitia chama kimoja cha siasa kukiwa na nidhamu. Taratibu za kulirudisha taifa mikononi mwa wananchi waliowengi zilianza kwa kuziandika kwa Kiswahili sheria, kannuni, katiba na kadhalika ili wote waelewe.



MAFANIKIO KATIKA AZIMIO LA ARUSHA
1.      Viwanda vilijengwa kuimarisha soko la kilimo, ushirika na mabwana shamba waliimarishwa.
2.      Ufundi wa asili uliokuwepo vijijini ulikuzwa toka vijijini hadi mijini, hapakuwa na tatizo kubwa la nguvu kazi/ vijana kuvikana vijiji vyao na kuhamia mijini walikotafuta maisha nafuu.
3.      Kulianzishwa viwanda vikubwa vya aina mbalimbali vikiwa mali ya umma, hata vile vya binafsi wennye viwanda hivyo waliwaheshimu na kuwapenda wafanyakazi. Mwaka 1980 hadi 1992 Tanzania kupitia SIDO na viwanda vikubwa tulibuni, kuchonga vipuri mbalimbali, kumimina vyuma(blocks) na kuunda injini na kadhalika.

4.      Uongozi imara ulioshika dola, serikalini ulitii na kupenda wananchi na wananchi pia walifanya hivyo kwa serikali yao; UPENDO, UMOJA, MSHIKAMANO, UTULIVU na AMANI tunayoitumia sasa pamoja na kuanza kuipaisha hapa ndipo ilijengwa sana. Hata wageni matajiri na masikini waliheshimiana.
5.      Mataifa ya kigeni walituheshimu na hatukua chini ya taifa lolote moja kwa  moja, tuliheshimika duniani kote.


6.      Tulikuwa na majengo ya kulaza watumishi wa umma kwa kiasi waliokuwepo, matumizi ya fedha yenye nidhamu yaliyojali mambo muhimu ya taifa na vipaumbele vyake.
7.      Hali hii iliharibika kiasi baada ya vita vya Uganda.  Hasa kwa kuwa hakukuwa na elimu ya uzalendo ya kuziba pengo, baada ya vita wananchi na wageni walionekana walibanwa na azimio la arusha  sio uzlendo wao.


KUONDOLEWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
1.      Baada ya vita ya Uganda kuliingia mteteleko wa utekelezwaji wa maazimio yetu kwakukosa elimu ya uzalendo wa kutuweka sawa.
2.      Mwaka 1986 harakati za uongezwaji wa pato la wananchi zilianza na ruksa ya kufanya mambo mengi lakini ndani ya azimio la arusha ulianza, lakini inadaiwa haikukumbukwa kuwekwa pato la taifa, uchumi wa taifa ulinza kuzolota; wakati baadhi ya wananchi hawana na kurudisha matabaka, rushwa na ufisadi viliibuka.

3.      Mwaka 1989 wazo la kulivunja azimio la arusha lilikomaa.

4.      Mwaka 1990 tuliitwa nikiwa katibu wa OTTU wa wizara ya ulinzi na majeshi la kujenga taifa, mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm la wizara hiyo na mjumbe wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Nia ya wito  ni kuangalia uhai wa chama (ccm) mahali pa kazi hususani AZIMIO LA ARUSHA nia kulivunja au kulibadilisha. Mkutano tuliufanyia karimjee hall.

5.      Niligundua kuwa kulikuwa kunadhaniwa azimio  lina tatizo au haliwezi kupokea mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
6.      Niliiwaambia kuwa azimio lenyewe halina matatizo ila mchanganyo wa watawala, wasimamizi, watendaji na watekelezaji wa azimio hilo ndio wamewekwa matatizo, haya ni matatizo ya kimfumo ya siasa tuurekebishe. NILIASA “TUKILIONDOA AZIMIO LA ARUSHA KAMA INAVYOONEKANA TUTAPATA MATATIZO MAKUBWA NA MABAYA SANA”.


MATOKEO YA KUONDOLEWA KWA AZIMIO LA ARUSHA
Mwaka 1991 azimio la arusha liliondolewa na kuzaliwa azimio la Zanzibar wakidai kupishwa MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA. Hapo zilizaliwa sera nyingi mpya zisizo na siasa juu yake; kwa vile sera huzaliwa na siasa basi ni wazi kuwa kuna siasa ya nje ya taifa Fulani tusiolijua walioitumia sera hizo na mifumo yake ya utekelezaji:
1.      Kukazuka sera ya UBINAFSISHAJI, UWEKEZAJI na UWEZESHWAJIi wa kigeni badala ya zile ZENYEJI. Zikaharibu na kuuza viwanda vikubwa, mashamba makubwa, viwanda vogovidogo mijini na vijijini, ni kama wameuwa muendelezo wa vipai vya ufundi na ubunifu wake vijijini na mijini lazima vipuri vyote vitoke nje.


2.      Imeuwa ushirika na huduma vijijini, vijana wengi wamevihama vijiji vyao na kuja kuwa wazurulaji mijini
3.      Taifa likakosa siasa yake ya kitaifa na sera zake, taifa likamegwa vipande vipande kiitikadi. Haijulikani vyama vyetu tunaviita vya siasa kwa siasa gain? Pengine hakuna siasa au kuna siasa ya makundi; kama hakuna siasa, hakuna wanasiasa, kunaweza kukawa na WAKEREKETWA, WANAHARAKATI na WATAWALA.
4.      Kwa kuwa utawala sio mali ya moja kwa moja ya wananchi iwapo hakuna uongozi wao imara, basi kundi la watawala wanaoendesha utawala wanaweza kugeuka watawala wa wengine au hata wakoloni mamboleo. Lakini kwa vile hauwi imara bila ya uongozi, lazima kundi hili litawaliwe na utawala unaoongozwa na uongozi wao, unaofuata siasa na sera zao, ambazo watawala (utawala) wetu watazifuata.
Kwa tabia ya elimu bora ya kuvuna ugenini na kupeleka ilikotoka lazima utawala wetu ufanye kila kinachotakiwa na wanaotawala.
5.      Hii ndio hatari kubwa tuliyonayo Tanzania na hata afrika nzima, kunawafanya wananchi kuhamisha mawazo yao kuyapeleka ugenini, kuiba maliasili, fedha, rasilimali na kadhalika kupeleka zikaendeleze watu na mataifa ya huko wanakodhani ndiko makwao.

UGUNDUZI WANGU
Huu ndio ukoloni mamboleo /ukoloni wa fikra unaotokana na ujinga wa kujikana, huu ndio ninaouita UGONJWA WA KIJAMII, tiba yake ELIMU YA UZALENDO niliyoigundua. Hii ni elimu mpya ninayoamini,
Tumeigawa katika miswada saba(7) nikipata fedha vitakuwa vitabu vya kuokoa taifa na bara zima a afrika…………….

JUMANNE A.MINDU
M/kiti wa AMALI NGO, Mgunduzi wa elimu hii na Mhandisi CRJE
AHSANTE

Monday, August 18, 2014

KATIBA MPYA YA NCHI NA WANANCHI.. TUIFANIKISHE



Mafanikio si kwa ajili ya watu waliochaguliwa na mungu pekee kama tunavyodhani, ila mafanikio huja kutokana na muendelezo wa mawazo chanya uliyojipangia kuyafanya ili kufanikisha ndoto zako uziotazo hata ukiwa unatembea... JITIHADA, UAMINIFU na KUSAIDIANA ndio nguzo stahiki kwa kila mtu...

yapaswa mjitahidi UKAWA kurudi bungeni na TANZANIA 1 pamoja na 201 kuweka tofauti pembeni kuzungumzia na kujadili yahusuyo nchi ili mfanikishe kutupatia KATIBA YA WOTE, KWENU VIONGOZI NA SISI WANANCHI...

TUNAWAOMBA...



ibrahim mindu (I.C.T ) Student kutoka UDSM (U.C.C)

ASALI NI DAWA TUITUMIE


KUJITIBU DALILI ZA KIKOHOZI KWA HARAKA

Wadau ukiona unajiskia dalili ya kikohozi na koo kukwaruza unaweza kuzuia kuumwa kwa haraka kwa kutumia mchanganyiko wa :-
1. ASALI(vijiko viwili vya chakula)
2.NDIMU/LIMAO(kijiko kimoja cha chakula)
3. MDALASINI WA UNGA (kijiko kimoja cha chai)
4. Changanya kwenye kikombe cha maji ya moto na kunywa ASUBUHI na USIKU kabla ya kulala.

Unaweza SHARE na wengine kuwajuza zaidi.

wakina mama

TUTAWEZALE KUJIKWAMUA IKIWA WAGAMBO, POLICE NA ULINZI SHILIKISHI WANATURUDISHA NYUMA KUFIKIA MAENDELEO TULIYOJIPANGIA?

Tupendane na kudumisha upendo kwaa kila mmoja awe masikini, wa hali ya kati ama wa matajiri... tulindane kufikia malengo...

KATIBA MPYA: HIVI TUTAFIKA KWELI AU NI KIZUNGU MKUTI AMBAYO TIBA YAKE TWAIFICHA KWENYE MIOYO YETU..!!!!?????

Tanzania ni tajiri  kwa  madini, maliasili, mazingira mazuri  yenye mipishano ya misimu ya mvua na mazao yanayomea  sehemu moja bila ya nyingine inayoruhusu uwepo wa soko kubwa la ndani mbali ya yale ya nje ya taifa hili, tukiogozwa na amani na utulivu.                                                                                                                                            
 Lakini  utajiri huu unashindwa kuuondoa umasikini wa taifa na mtu mmoja mmoja  kwa waliowengi. Viongozi wanahaha kukitafuta kikwazo chake, wakibadili badili  mfumo, sera na mipango bila ya mafanikio ya kukigundua.        
                                                                                                                                                               Mwaka  1987 – 2002 nilikitafiti kikwazo hicho, nilikigundua pamoja na kiini chake, kilipofichwa na namna ya kukiondoa ili tupige hatua. Tukiwa  AMALI NGO kwa kuyatumia matokeo hayo  mwaka  2002  tuliliarifu taifa kuwa dawa za asili ni sayansi ili tupate ufunguo  wa kuwaangaza watu kwenye asili yetu kilikofichwa kikwazo hicho, hatukuhusishwa, sheria  no.23 ya mwaka  2003 haitimizi lengo. 
             
 Ugunduzi huu unahitajika sana hivi sasa ambapo athari za kikwazo hicho zinaharibu mchakato wa katiba mpya, zinatunyima siasa na uongozi wa kitaifa ambao ungemaliza hata tatizo la msingi  la muungano wetu lililojificha, pia zinatishia kuvuruga  AMANI, UTULIVU, MSHIKAMANO, UMOJA, HURUMA YETU, USAWA na HAKI  vinavyoficha siri iliyomo kwenye mchakato wa KATIBA MPYA.                                                                                                       
Katika kuwatafuta wanaolitakia mema taifa hili ili watushike mkono kwa hali  na mali tuweze kukisema kikwazo hiki  na athari zake  kwa nyanja zote za taifa letu, kisha tutoe elimu tujiokoe. Kwa muda mfupi  nimegundua kuwa wewe ni mmoja  wa hao tunaowatafuta, hivyo nakuomba utusaidie ili ushiriki katika kuliokoa taifa  letu, ubakie kwenye utajo na historia ya taifa na bara letu  kwakuwa hiki ni kikwazo cha bara  zima, huku ukifaidika.


                                                                                                                                                                                                                      BW  . J . Mindu
M / Kiti  wa AMALI NGO, Mgunduzi wa hili na  mhandisi   

Monday, July 14, 2014

BARUA YA WAZI KWA WAHESHIMIWA MARAIS DAKTA. J .M. KIKWETE NA DAKTA. A .M.SHEIN



              BARUA YA WAZI KWA WAHESHIMIWA MARAIS  DAKTA. J .M. KIKWETE  NA  DAKTA. A .M.SHEIN



      YAH:  KUWAOMBA MLINUSURU BUNGE LA KATIBA MPYA LITIMIZE               LENGO KUSUDIWA
  


Tafadhalini waheshimiwa husikeni na ombi la hapo juu mkiwa wakuu wa taasisi ya siasa ya umma au umma wa Taifa letu, ninyi si serikali wala wakuu wa vyama vyenu tu.

Inaonekana  Mungu ameamua kutukomboa dhidi ya adui yetu mkuu ukoloni mamboleo aliyetajwa mwaka 1967, bila ya ufafanuzi wake. Adui huyu yumo ndani yetu na ndani ya mifumo yetu ya maisha ,uongozi na utawala kwa ngazi ya Taifa na bara letu. Tusipomuondoa anaweza kuturudisha kwenye ukoloni au utumwa wa awali polepole.

Mungu anajua kuwa chini ya adui huyu hatuwezi kuyatimiza malengo ya uhuru wetu tuliyoyataja mwaka 1961,1964  na 1967 hata tukiwa chini ya uongozi na utawala wa chama kingine. Anafahamu kuwa tuliarifiwa juu ya uwepo wa adui huyu bila ya ufafanuzi,  huenda wasemaji hawakumfahamu vema adui huyu kwa vile nao walikuwa kundi la pili la wafuasi wa waasisi wa harakati za kuutafuta uhuru wetu waliomjua vema adui huyu.

Kama alivyowafanya waliotangulia, Mungu anawainua ninyi bila ya kulijua lengo la kuzianzisha harakati za awamu ya tatu ya ukombozi wetu dhidi ya adui huyu, anawaongoza kuanzisha mchakato wa kulikagua Taifa letu toka tulikoanzia, tuone tulipopotelea tujikosoe tutunge na kuandika katiba mpya itakayotuongoza katika harakati za ukombozi wetu bila ya kuijali baadae yenu,  kwa amani na utulivu wenye mshikamano na umoja. Ndio maana mwaka 2002  tukiwa AMALI NGO tuliishawishi serikali na WHO wakatunga sheria no 23. ya mwaka 2003 ya tiba asili, tulikuwa tunatengeneza ufunguo wa kuingilia alikofichwa adui huyu. Tuko tayari kutoa elimu ya kina kwa umma, uongozi na serikali dhidi ya adui huyu na harakati hizi nzito. 

Amewajaza hekima, busara na upendo kwa Taifa letu, mkautumia ufunguzi wa bunge la katiba mpya kuyavua madaraka na ushawishi wa uraisi ,serikali ,vyama vya siasa, tume na uandishi wa rasimu za katiba mpya, mataifa ya nje taasisi za dini, asasi za kiraia na mtu mmoja mmoja mbele ya bunge la katiba mpya ; sote tuwe watoa maoni yenye mifumo ya hoja zijadilike kwa maridhiano, hivyo ndivyo waraka wa kisiasa au katiba ya taifa itakavyopatikana

Hili bunge maalumu tofauti na mabunge ya kawaida, litakuwa na wajumbe bila ya miswada,waraka wa rasimu ya pili ya katiba mpya utakuwa waraka wa maoni kiongozi yaliyowekwa kwenye mifumo ya hoja yaongoze mijadala. Mfumo huu unawataka wajumbe kuwa wamoja waingize mambo yaliyosahaulika au yasiyoandikwa kwenye rasimu au kuleta maoni mbadala yakiwa kwenye mifumo ya hoja ili kwa hekima na busara zao waunde katiba bora. 

Kwa bahati mbaya harakati za awamu ya tatu ya ukombozi wa Taifa letu zilizofichwa ndani ya mchakato wa uandishi wa katiba mpya hazikutangazwa pamoja nao, huenda siri hii ya Mungu haijajulikana. Hivyo wajumbe wa bunge hili waliuona mchakato huu ni zawadi kwa muungano wetu kutimiza miaka 50 tunatafuta namna mpya ya ugawanaji mamlaka na madaraka ya taifa letu au tunatafuta aina mpya ya maisha au ustawishaji taifa. Katika mvutano huu wa fikra walijenga misimamo iliyowagawa, rasimu waliigeuza kuwa mswada baada ya maoni kiongozi; ukawa na wenyewe, wapinzani na waliotupwa nje. Kwa kuwa tendo hili ni nje ya taratibu za bunge   hili wakajikuta kila upande ukitoa matamko yasiyoweza kujadilika badala ya kutoa hoja za matamko hayo ambazo zingewapeleka hadi kwenye viini vya matakwa yao kama vile BMZ, SMZ, TAMISEMI na kadhalika; kasoro hii imelifanya kundi moja liamue kujitoa bungeni.

Kwa kuwaambia siri ya Mungu aliyoificha kwenye mchakato huu naamini sasa mtakuwa mmeelewa kuwa kinachotarajiwa kufanywa hapa ni zaidi ya katiba. Tunataka wajumbe wabakie wamoja wajenge nguvu ya utaifa na rasimu iwe maoni kiongozi ili yaruhusu maoni mapya yatakayojadiliwa sambamba na maoni kiongozi kwa nyanja husika, ikibidi hekima, busara , sheria na sera tulizoziacha za waasisi wetu tuziite katika kuifanikisha siri iliyofichwa kwenye mchakato huu. Hivyo natarajia wajumbe wote bila ya makundi wala misimamo au masharti nawasihi mrudi bungeni mkalijenge upya taifa letu msahau mliyonayo.


Nimeigundua siri hii katika utafiti nilioufanya toka mwaka 1987 -2002 nikitafuta kiini cha vikwazo vya taifa letu tajiri kwa utalii, rasilimali na mali asili, vipaji vya sayansi na ufundi mbali ya vya ustareheshaji, ardhi bora na kubwa yenye uzalishaji  wa kutosha, lakini hatujitoi kwenye umasikini, tunazidi kuwa tegemezi sasa hatuna siasa / dira, uongozi na serikali ya kitaifa , nyumba za kulaza watumishi, viwanda na kadhalika, pia kwa kukikana Kiswahili hadi leo taifa halijarudishwa kwa wananchi waliowengi maarifa tunayoyapata kwenye mataifa ya nje hatuyafikishi kwa wananchi waliowengi yakatuletea maendeleo, hatujui aina /mfumo wa elimu bora kwetu yakutukwamua tulipokwama, mbali ya hayo adui huyu ameharibu dhana yetu ya uwazi uwajibikaji, na ushirikishwaji  kwa kupunguza mamlaka ya raia dhidi ya uongozi wao na uongozi dhidi ya utawala /serikali yao kunakozaa rushwa ,ufisadi, ulegevu wa ulinzi wa mipaka, kupoteza huduma kwa umma, kujinyima fedha kitaifa na kadhalika. 


Mambo haya niliyawasilisha juu juu kwa taifa  kupitia ITV mnamo tarehe 26/04/2012: mada: NINI TANZANIA, ASILI NA HALI YAKE MIAKA 48. Tarehe 30 /04/2012: mada: TOFAUTI YA ELIMU YA UZALENDO NA ELIMU YA URAIA na tarehe 27/03/2914: mada: UGUMU WA KUUNGANISHA SERIKALI ZA TAIFA LETU;  naziona serikali za jamuhuri ya muungano wa Tanzania na TAMISEMI za kiraia lakini BMZ na SMZ za kijeshi,  vipi zote zitakuwa za kiraia ziwe na sura moja ziunganishwe? Adui huyu kwa miaka yote amewazuia viongozi wetu kulirekebisha hili kiasi inaonesha  CCM ina serikali ya muungano na tamisemi ya Tanganyika /Tanzania bara lakini upande wa Zanzibar / Tanzania visiwani  hupata wawakilishi kutokaBMZ wenye serikali  SMZ na kuwaingiza kwenye bunge na serikali ya muungano.




Kwa ufafanuzi huu wa kitafiti ni wazi watanzania wote sasa tutajua tunachotarajiwa kufanya kwa ajili ya salama yetu,  kumshukuru Mungu kwa ufunuo huo ni kwa wajumbe wote kurudi bungeni na tulionje tuwasaidie, maana hii ni vita dhidi ya adui yetu mkuu ukoloni mamboleo ila tujue adui huyu hakuumbwa ameundwa/kubuniwa na watu kwa maslahi yao. Wajumbe mkija na msimamo, mkisusa bunge, mkikataa kujadili yaliyonje ya rasimu, mtakuwa mnamsaidia adui huyu na waliomuunda kutekeleza malengo yao na kuliangamiza taifa na bara letu


 
J4mindu@gmail.com , 0753746479, 0787746479
mindujr3@gmail.com , 0719554564,


Wenu mtiifu
J .A. Mindu`
Mgunduzi, m/kiti wa AMALI NGO na mhandisi