Mwaka 1979 watanzania tulikuwa kwenye furaha kubwa ya ushaidi wa vita dhidi ya Iddi Amin, japo kwenye baadhi ya miji kulionekana kama kungekua na ugumu kiasi cha kuifanya serikali kuchukua tahadhali kwa kuwawekea askali wengi wa JKT mitaani.
Kumbe vita hivi vilitusaidia watanzania kuuona umuhimu wa amani, utulivu na kuwa na vyetu kitaifa na binafsi kama sera za siasa yetu asilia zinavyotuelekeza kujenga utashi na uthubutu wenye kujiamini wa kuzitafsiri elimu za kigeni tulizozipata kwenye vitendo. Tulianza kuwa wabunifu; kuna waliobuni mashamba makubwa, zana za kulimia kama plau, vipuri vya magari, matrekta na machine mbalimbali za usagaji na umwagiliaji za gharama nafuu, pia uundaji wa silaha za kisasa zilizolingana na zilizoletwa vitani, hali hii ilijitokeza mijini na vijijini.
Cha kushangaza wasomi viongozi na watawala wa kitanzania hawakuyaenzi matokeo haya kama mavuno ya vita, wakayaacha yakapita, viwanda na ardhi walizokuwa wakizitumia wabunifu hao vilizolota, kuuzwa na kuwekezwa kwa wageni na wabunifu wenyeji kufukuzwa. Nikajiuliza iwapo kwenye vita hivi kilichotuponya ni kuwa na vijana wetu na vyetu je vipi hawa wanaonyesha moyo wa kuiongeza hawakusaidiwa? Vipi hivyo vyetu vichache baada ya vita kwanini havikuboreshwa kutokana na msaada vilivyouonyesha? nilihisi huenda vita vile vilikua njama ya kututoa nje ya njia sahihi ya maendeleo yetu. Huenda wamefanikiwa kama kweli basi uhuru wetu haukuwa na elimu ya asili yetu ya kutukinga tusitolewe kwenye njia yetu, dalili zikaonyeshwa hata baada ya miaka mingi toka vita hatukuwa na elimu asilia ya kututibu na kuturudisha kwenye njia sahihi ya dhamira ya uhuru wetu na kutufikisha kwenye taifa letu la AHADI tuliloamua kuliita Tanzania.
Nilipoangalia nyuma sana niliuona mchoro dhaifu (grafu) ya makuzi na maendeleo yetu sio nzuri, Hapa niligundua kuwa hatuna elimu ya asili yetu ambayo ndio ingetupa elimu tiba na kinga, nikapata hofu kuwa uhuru wetu hauna kinga, basi pia hatukijui kiini cha utumwa na ukoloni wetu na namna ya kukiondoa.
Mwaka 1987 – 2012 nilianza kufanya utafiti na uchambuzi kukitafuuta kiini hicho, elimu ya kukiondoa kuturudisha kwenye njia yetu ya makuzi bora na maendeleo kulingana na dhamira/ahadi ya uhuru wetu na kinga dhidi ya kurudishwa tulikotoka, kwani wazee wetu nao waliingizwa huko kwa mbinu kama hizihizi.
Utafiti huo nimeufanya kwa jina la opereshi JAM, yaani siagi inayopaswa kuwekwa kwenye mkate Tanzania ili watanzania wenyewe waifaidi nchi/taifa lao. Mradi huu niliufanya bila ya hadidu rejea niliamua kuufanya kama kamali, nikishinda nitaomba fidia kwa serikali kwa kuwa hili ni jambo la kitaifa na kibara sana, nikishindwa basi. …